Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JICA yaisaidia ZAWA kuboresha miundombinu maji

$
0
0
Na Amina Masoud, MCC
MKURUGENZI wateja kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Nd. Mussa Ramadhan Haji ameishukuru Kampuni ya Japan International 
Cooperation Agency (JICA), kwa misaada inayowapatia.

Mkurugenzi Mussa aliyasema hayo baada ya Kampuni hiyo kupitia walimu wa taaluma kutoka Japankuwatembelea kwa lengo la kukagua miradi inayoendesha na Mamlaka hiyo.

Alisema JICA kwa miaka mingi inaisaidia Zanzibar kupitia mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kwa kuwapatia miundombinu ya maji ya uhakika.
Katika ziara hiyo, Walimu hao walitembelea ZAWA na kujionea jinsi misaada waliyoitoa inavyofanyakazi na kuwafikia walengwa.

Alisema ugeni huo uliambatana na ziara ya kutembelea visima vilivyojiengwa kwa udhamini wa kampuni hiyo ili kujua namna vinavyosaidia wananchi.

Ziara hiyo ilianza kwa kutembelea chemchem ya maji iliyopo Mtoni, tangi la maji lililopo Dole Wilaya ya Magharib lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni moja na laki mbili na huyasambaza katika wilaya ya Magharibi Unguja.


Maeneo mengine waliyotembelea ni pamoja na visima vya maji Welezo venye uwezo wa kuhifadhi maji zaidi ya lita milioni nne, tenki la kinuni lenyeuwezo wa kuingiza maji milioni mbili na laki saba pia walifika kwenye tangi kubwa la maji Saateni.

Aidha Mkurugenzi Mussa alieleza ujio wa ugeni huo ulikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya watu wa Zanzibarna Japan ambapo pia kampuni hiyo inatarajia kujenga soko la kushushia na kuuzia samaki kutoka Japan, sambamba na kuchukua baadhi ya Wazanzibai kwenda kusoma Japan ili kazidisha uhusiano wao.


Alieleza mradi huo ulioanza tokea mwaka 2006 umetenga fedha taslimu za kutaka kuiisaidia mamlaka ya maji ZAWA ili kuendeleza shuhuli zake za kuwasaidia wananchi, sambamba na kuboresha miundo mbinu ya maji nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>