Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wanasiasa wahusishwa mauaji ya albino

$
0
0
Na Farida Msengwa, Morogoro
WANASIASA wametajwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika ukatili na mauaji yanayofanywa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ili kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na gazeti hili ofisi kwake,Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Morogoro (TASI), David Mganga, alisema chama kilifanya uchunguzi na kubaini kwamba mauaji na ukatili dhidi ya albino yanaongezeka zaidi katika kipindi cha karibu na uchaguzi.

Alisema matukio ya mauaji na kunyofolewa viungo kwa watu wenye ulemavu, yalishamiri mwaka 2009 na kuanzia mwaka 2010 lakini yalipungua mwaka 2011.


Aidha alisema yameanza kuibuka tena mwaka 2014 na kwamba kama hayatadhibitiwa yataendelea kuongezeka hadi mwishoni mwa mwaka ujao.

Alisema ingawa wanaokamatwa na viuongo vya albino ni  watu wa kawaida lakini wamebaini kuwa kuna wakubwa nyuma yao ambao wamekuwa wakiagizwa kufanya ukatili huo.

“Hawa wanaokamatwa ni kumbikumbi tu, wanaagizwa na viongozi wenye malengo ya kutimiza malengo yao kisiasa ,” alisema.

Alisema mtu wa kawaida hawezi kuwa na mahitaji ya viungo vya albino, isipokuwa viongozi wa kisiasa na matajiri ndio wanaowatuma ili kujinufaisha.

Aliitilia shaka kampeni iliyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009-2010, kupiga kura ya siri kuwatambua wauaji wa albino akisema ni ya kisiasa.


Alisema baada  ya kampeni hiyo hakukuwa na mrejesho wowote na kusema huenda mrejesho haukuwa mzuri.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>