Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Waziri wa Afya na Naibu wake watembelea Vitengo vya Hospitali ya Mnazi Mmoja.

$
0
0
Na Ramadhani Ali --Maelezo.
Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja  inayojumuisha Hospitali tatu, Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja, Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu na Hospitali ya Wazazi ya Muembeladu Dkt. Jamala Adam Taib amesema kazi kubwa inayofanywa na Idara hiyo katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2010 ni kuimarisha Hospitali ya Mnazimmoja ifikie kiwango cha Hospitali ya rufaa.

Amesema hatua zinazochukuliwa na Idara  ni Kuimarisha miundo mbinu, kusomesha wataalamu wa fani tofauti za afya, kuimarisha uchunguzi wa maradhi na kuhakikisha madawa yanapatikana katika Hospitali hiyo.

Dkt. Jamala amemueleza Waziri mpya wa Wizara ya Afya Rashijd Seif Suleiman alipofanya ziara ya kutembelea Hospitali hiyo kuangalia utendaji wa kazi na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.

Amesema majukumu yote waliyopangiwa katika  kuimarisha Hospitali Kuu ya mnazimmoja wamefikia hatua nzuri na hivi sasa wananchi wamejenga matumaini makubwa kutokana na huduma zake.

Dkt. Jamala  amesema Idara ya Hospitali ya Mnazimmoja  inawafanyakazi 800 wakiwemo madaktari bingwa 14 na   Serikali inaendelea kusomesha wataalamu wa fani mbali mbali ambapo wanafunzi 200  wa fani ya udaktari wapo vyuoni .

Pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, Dkt. Jamala amesema bado inakabiliwa na ufinyu  mkubwa wa bajeti na mageuzi yanayoendelea ya kuifanya   Hospitali hiyo  iwe inajitegemea.

“Changamoto hizi hata hivyo haziathiri malengo yetu ya kuwapa wananchi matumaini ya kupata huduma  bora katika Hospitali hii,” Dkt Jamala alimueleza Waziri wa Afya.


Msaidizi Mganga Mkuu wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Muhidini Abdalla Muhamed amemueleza Waziri wa Afya ambae alifuatana na Naibu wake Mahmoud Thabit Kombo kwamba kliniki  ya meno ya Hospitali hiyo inavifaa  vya kisasa kutoka Shirika la MCW la Marekani na kuifanya kuwa kliniki bora zaidi  kuliko hospitali nyengine za Zanzibar.

Amewahakikishia wananchi kwamba huduma za matatizo  yote ya meno zinapatikana kwenye kliniki hiyo na kuwataka wananchi kutokuwa na wasi wasi na waendelee  kuitumia.

Katika kitengo cha maradhi ya kisukari daktari msaidizi wa maradhi hayo Dkt. Miskia Ali Mohd alimueleza Waziri  kwamba maradhi hayo yanaongezeka kwa kasi na kumekuwa na upungufu mkubwa wa dawa za maradhi hayo.

Amesema tatizo jengine linalokabili kitengo hicho ni upungufu wa chakula cha wagonjwa wa kisukari wanaolazwa katika Hospitali hiyo ambacho kinatakiwa kiliwe sambamba na matatibabu wanayopatiwa ili dawa  wanazotumia zifanyekazi  kwa ufanisi.

“Naiomba wizara ifanye juhudi za  kuhakikisha dawa za  maradhi ya kisukari  na chakula maalum cha wagonwa wanaolazwa  vinapatikana kwani  maradhi haya  yamekuwa hatari zaidi hata kwa watoto wadogo, ”alisisitiza Dkt. Miskia.

Waziri wa Afya kwa upande wake amewataka viongozi  wa Idara hiyo kuimarisha umoja na  mshikamano  na watendaji  wao ili kufanikisha malengo yaliyowekwa  ya kuwahudumia wananchi na kuwapa huduma nzuri.

Ameupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kuanzisha utaratibu maalum wa kuangalia wagonjwa waliolazwa ambao umepunguza msongamano wa watu katika mazingira ya sehemu hiyo.         

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles