Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Maalim Seif:Ukosefu sera wachangia migogoro wafugaji, wakulima

$
0
0
Na Khamis Haji, OMKR
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema migogoro inayowakumba wakulima na wafugaji na kusababisha mauaji inasababishwa na serikali kukosa sera sahihi ya kilimo na ufugaji.

Aliyasema hayo katika mikutano tafauti akiwa katika ziara ya siku nne mkoani Mwanza kwa ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo iliyo chini ya kata zinazoongozwa na CUF pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara. 

Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua daraja katika kata ya Igogo, alisema inasikitisha kuona kila siku wakulima na wafugaji wakiuana kwa kugombea maeneo ya kilimo na kulishia mifugo huku serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo.

Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema kusingekuwa na mauaji kati ya wakulima na wafugaji iwapo serikali ingekuwa na sera thabiti inayoanisha maeneo maalum kwa ajili ya ufugaji na wakulima.


Alisema Tanzania imejaliwa maliasili nyingi kuliko nchi nyingi duniani na iwapo zingeweza kuzitumika vizuri hakuna sababu nchi kuwa miongoni mwa nchi masikini.

Alisema mbali na maliasili zilizopo chini ya ardhi kama vile madini, gesi na mafuta, Tanzania imejaaliwa kuwa na hali ya hewa inayotafautina katika maeneo ambayo inaifanya nchi kuzalisha mazao tafauti tafauti.

Hata hivyo, alisema kukosekana kwa sera muafaka kunasababisha wananchi walio wengi kushindwa kunufaika na neema hiyo na kutoa mfano, licha ya wananchi wa kanda ya Ziwa kuongoza kwa kilimo cha Pamba, lakini hakuna hata kiwanda cha nguo.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha Kirumba, alisema wananchi hawana budi kujiandaa kufanya mageuzi ya uongozi wa nchi kwa kuwaweka madarakani viongozi wenye uwezo na mtazamo mpya wa kuleta maendeleo ya wananchi.

Naye Mbunge wa Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekiel Wenje, akihutubia katika mkutano huo alisema njia muafaka ya kuleta mageuzi ya kiuongozi nchini ni vyama vya upinzani kuendeleza ushirikiano na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.

Alisema yeye binafsi yuko tayari kufadhili safari ya viongozi wakuu wa CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi wakajifungie nchini Sychelles ili waweze kupata mgombea mmoja ambaye watamsimaisha kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani kupitia Ukawa.


Hata hivyo, akilifafanua hilo, Maalim Seif alisema jambo hilo wala halihitaji kwenda kuamuliwa nje ya nchi, na badala yake viongozi hao wanaweza kutoa maamuzi hayo hapa hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles