Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Waandishi kutoka Bara, Uganda na Zanzibar watembelea mkoa wa Lindi kukagua shughuli za Gesi

$
0
0
 
AFISA Rasilimaliwatu wa Halmashauri wa Kilwa mkoani Lindi, Charles Mwaitage akizungumza na waandishi wa habari wa nchi za Tanzania Bara, Uganda na Zanzibar walipofika afisini kwake, kabla ya kuanza ziara ya kutembelea harakati za uchimbaji wa gesi uliopo Kata ya Songo songo (picha na Haji Nassor, Lindi)

 
, WAANDISHI wa habari wa Tanzania Bara, Uganda wakionyeshana maelezo yaliopo kwenye kikuta maalumu kilichowekwa ili kukitambua kisiwa cha Kilwa, halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi kuwa kimeingia kwenye urithi wa kimataifa, ambapo kisiwa hicho kilikaliwa na waswahili tokea karne ya 9, sawa na miaka 1200 iliopita kasha kuhamiwa na watawala wa Oman karne ya 14 na 15 (picha na Haji Nassor, Lindi) 

 MOJA kati ya makaburi waswahili yafikayo 80 yaliopo Kilwa kisiwani, halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi, ambapo yamekuwa hapo tokea karne ya 9, (miaka 1200 iliopita) kabla ya karne ya 14 na 15 kisiwa hicho kuhamiwa na wareno na waarabu kutoka Oman, kwa kufuata dhahabu na pembe za ndovu (picha na Haji Nassor, Lindi)
 
MABOMBA maalumu ya kusafirishia gesi asilia yenye upana wa nchi 36, ambayo yanatarajiwa kufukiwa kuanzia mkoa wa Mtwara hadi mkoani Dar –es Salaam zaidi ya kilomita 500, kazi ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Disemba mwaka huu, chini ya shirika la maendeleoa ya mafuta ya Petroli Tanzania TPDC na kampuni moja kutoka Afrika kusini (picha na Haji Nassor, Lindi) 

 
MKUU wa mkoa wa Mtwara kanali mstaafu, Joseph Loen Simbakalia, akiwaelezea waandishi wa habari wa Tanzania, Uganda na Zanzibar  mikakati ya mkoa juu ya matumizi ya gesi asilia iliopo mkoani humo (picha na Haji Nassor, Mtwara)

 
KAIMU mkuu wa bandari ya Mtwara Musiiba Fikiri (kulia) akiwa na waandishi wa habari wa Tanzania, Uganda na Zanzibar wakitembelea bandari hiyo, ili kuona shughuli zinazvyoendelea bandarini hapo na hasa baada ya Mtwa kugundua gesi mwaka jana (picha na Haji Nassor, Mtwara)



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>