Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mnazimmoja yakiri wagonjwa kupatiwa chakula

$
0
0
Na Khamisuu Abdallah
Wizara ya Afya imesema bado inaendelea na utaratibu wa kugawa chakula kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali zake zote.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Mmnazimmoja,Katibu wa hosptali hiyo, Hassan Makame Mcha, alisema utaratibu huo bado upo lakini kwa mujibu wa bajeti chakula hicho kinatolewa kwa wagonjwa wasio na ndugu.

Aidha wagonjwa hao upatiwa mlo wa mchana pekee lakini hali ya fedha inaporuhusu hupatiwa mlo kamili.

Hata hivyo, alisema hali ni tofauti kwa hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu, ambao hupewa chakula mara tatu.

“Kwa kweli tunaowaangalia sana ni wale wagonjwa wa Kidongochekundu kutokana na hali zao, wale tunawapa mlo kamili lakini kwa hospitali zetu mbili tumekuwa tukitoa mlo mmoja  tu kwa wale wagonjwa ambao hawana ndugu,” alisema.


Alisema tayari wameshaanda bajeti  ya chakula kwa wagonjwa na ikipata ridhaa wataendelea kutoa mlo kamili kwa wagonjwa wote wanaolazwa katika hospitali zao.


Aliwaomba wananchi kuendelea kuzitumia hospitali zao kwani nia ya serikali ni kutoa matibabu bora kwa wananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>