Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

IGP Mangu ataka wahalifu wafichuliwe

$
0
0
Na Kija Elias, Moshi
Jjeshi la Polisi limewataka wananchi kutoa taarifa sahihi juu ya uhalifu ambao umekuwa ukijitokeza nchini.

Kauli hiyo imetolewa na IGP, Ernest Mangu, wakati akizindua kituo cha polisi Majengo, Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,  kilichokarabatiwa kwa nguvu za wananchi, ambapo zaidi ya shilingi milioni 44 zimetumika.

“Jeshi la polisi haliwezi kulinda raia na mali zao kama hakuna ushirikiano baina ya wananchi na jeshi hili,hivyo ninachowaomba wananchi muendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi,”alisema.

Alisema suala la uhalifu bado ni tatizo kubwa, hivyo aliwataka wananchi  kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuweza kupunguza uhalifu huo.


Alimwagiza Kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boas, kuhakikisha kituo hicho kinatoa huduma bora bila ya kuwa na upendeleo kwa wananchi, kwani ndilo deni ambalo wananchi wamelikabidhi kwa jeshi hilo.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa za askari polisi wanaojihusisha na vitendo viouvu ili aweze kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza.

Katika hatua nyingine, IGP Mangu, alipata fursa ya kuzindua jengo la dawati la jinsia na watoto la wilaya ya Moshi ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 117.


Awali kitoa taarifa kwa Mkuu wa polisi nchini, Kaimu Kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, alisema kituo hicho kilijengwa enzi za mkoloni, hivyo kilikuwa kinavuja wakati mvua zinaponyesha na kushindwa kutoa huduma.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>