Na Husna Sheha
KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk.Khalid Mohammed, amesema serikali inatafuta vifaa vya kisasa kukabiliana na maafa.
Alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa vyama vya siasa katika warsha ya kukabiliana na maafa iliyofanyika hoteli ya 0ceaon View, Kilimani Zanzibar.
Alisema serikali ya Zanzibar imeona umuhimu wa kuimarisha mikakati ya kukabiliana na majanga ili maafa yatakapotokea athari yake isiwe kubwa kwa jamii na taifa.
Muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Joseph Mayunga, aliwaasa wanasiasa kuacha na utashi wa kisiasa na chuki na badala yake kuunda mpango mkakati wa kukabiliana na maafa ili kuepusha majanga.
Aliwaomba kuitoa taaluma waliyoipata kwa wanachama wao na kuwahimiza kutunza rasilimali za nchi ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.
Nao washiriki wa warsha hiyo, waliishauri serikali kujenga nyumba maalum ya kuhifadhia maiti ili kuepusha usumbufu wakati majanga yanapotokea.
Warsha hiyo ilitangulia na dua ya pamoja ya kuwaombea waliopatwa na maafa ya kuzama na meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea mwaka 2011.