Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tumbe wapiga marufuku kuuza samaki wa kuzamia Ramadhani Wakanusha wavuvi Tumbe kuzuiwa kuuza samaki.

$
0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
VIONGOZI wa kamati ya maadili na Mashekhe katika shehia ya Tumbe, wamesema hakuna mvuvi aliyefukuzwa ama kuzuiwa kuvua na kuuza samaki katika bandari ya Tumbe.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wamekanusha taarifa zinazotolewa na baadhi ya wavuvi kwamba wamefukuzwa na kuzuiwa kuvua na kuuza samaki katika bandari hiyo na kusema walichozuia ni kuuza samaki wa kuzamia wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Walisema kutokana na imani za kidini ni kosa kuzamiwa wakati wa Ramadhani na kusisitiza kwamba wananchi wa Tumbe wako tayari kushirikiana na wavuvi wanaokuja kwa shughuli za uvuvi katika bandari yao lakini uamuzi wa kuzuia kuuza samaki wa kuzamia kila ifikapo  Ramadhani uko pale pale.

Katibu wa Kamati ya maadili, Seif Juma, alisema kabla hawajachukua hatua za kuzuia kuuzwa samaki wa kuzamia katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani, walikutana na wavuvi waliokuweko dago na kuwataka wasiuze samaki wanaowavua kwa njia hiyo.

"Sisi hatukukurupuka, kwanza tulikutana na wavuvi mwezi 28 kabla ya Ramadha ni, tulifanya hivyo ili kulinda na kuheshimu mwezi wa Ramadhani tunashangaa kusikia wamefukuzwa,” alisema.


Naye Shekhe Mbwana Dawa, alisema kwa mujibu wa dini ya kiislamu, Waislamu wametakiwa kuchukia mabaya yanayotendeka machoni au kuyakataza kwa mikono na kwamba wanaozamia swaumu zao hazikubaliki.

Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Tumbe, Sharif Ali Khamis, aliwataka wavuvi kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na kusema taarifa za kufukuzwa na kuzuiwa kuuza samaki si za kweli.


Alisema wananchi wa Tumbe wanatambua mchango wa sekta ya uvuvi katika kuchangia pato la taifa na wananchi wake na kuwataka wavuvi kuondoa dhana hiyo potofu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles