Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Serikali yashauriwa kuondoa muhali kumaliza dawa za kulevya

$
0
0
Na Khamis Amani
Serikali imeshauriwa kuondoa muhali katika utatuzi wa changamoto mbali mbali zinazozikabili jamii, ili ziishi kwa usalama na amani na ziweze kufanikisha maendeleo ya familia zao.

Sheha wa Shehia ya Kwahani wilaya ya mjini Unguja, Nassir Ali Kombo, aliyasema hayo ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya matatizo yanayoikabili shehia hiyo.

Alisema shehia hiyo ni moja kati ya shehia zilizokumbwa na wimbi la vijana wanaotumia dawa hatari za kulevya, ambazo husababisha ongezoko la matukio ya kihalifu ambayo ni hatari katika ustawi wa maendeleo ya maisha ya jamii.

Alisema, japokuwa dawa za kulevya ni janga la taifa lakini serikali inapaswa kuondoa muhuli kwa kuwadhibiti wale wote wanaoingiza dawa hizo, ili kuwanusuru vijana ambao ndio nguvu kazi ya familia na taifa kwa ujumla.


Alisema shehia ya Kwahani ni moja kati ya shehia zilizokumbwa na kadhia hiyo kutokana na baadhi ya vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo, na kupelekea kuwepo vitendo vya uhalifu.

Alisema, wengi wa vijana wanaotumia dawa hizo wamekuwa wakikosa imani ndani na nje ya familia zao kutokana na vitendo viovu wanavyovifanya.

Aliiomba serikali kuondoa ukimya kwa kuwadhibiti wale wote wanaongiza dawa hizo kuliko kuwakamata wauzaji wadogo.


Aidha aliwaomba wananchi wote wa shehia hiyo kuweka mazingira yao katika hali ya usafi hasa katika kipindi hiki cha mvua, ili kujikinga na maradhi ya miripuko yakiwemo matumbo ya kuharisha.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles