Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

NIDA yaanza kugawa vitambulisho kwa wananchi

$
0
0
Na Juma Khamis
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ofisi ya Zanzibar, imeanza zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa wilaya ya kaskazini ‘A’ Unguja.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkurugenzi wa NIDA ofisi ya Zanziba, Vuai Mussa Suleiman, alisema vitambulisho hivyo vinatolewa kwa utaratibu maalum uliowekwa.

Shehia ambazo vitambulisho hivyo vitaanza kutolewa ni Bandamaji,Kinyasini,Kandwi,Pwani Mchangani,Kisongoni,Matemwe, Kivunge,Mkwajuni, Kidombo,Kidoti , Moga, Gamba na Muwange.

Alisema vitambulisho vitatolewa kwa siku tano kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo wananchi ambao majina yao yamo kwenye orodha watatakiwa kwenda kwenye vituo vyao walivyojiandikisha.

Kwa upande wa utoaji wa vitambulisho kwa maidara na taasisi za serikali kisiwani Pemba alisema limeanza jana.

Aliwataka wananchi wanapokwenda kuchukua vitambulisho vyao wachukue stakabadhi walizopewa wakati wa kujiandikisha na kama zimepotea wachukue vitambulisho vyengine walivyovitumia wakati wa kujiandikisha.


Aidha alisema NIDA tayari imeshafungua  ofisi katika wilaya zote za Zanzibar isipokuwa wilaya za kaskazini B Unguja na kusini ambazo hazijakamilisha masuala ya kiutawala.

Alisema lengo la kufungua ofisi hizo ni kuwahudumia wananchi ambao hawakuwahi kusajiliwa wakati wa zoezi la awali.

Hata hivyo, alisema NIDA inakabiliwa na changamoto mbali mbvali ikiwemo wananchi kutotumia fursa ya kupelekewa vitambulisho vyao katika maeneo wanayoishi badala yake wanalazimika kuvifuata ofisi za wilaya.

Pia alisema baadhi ya wananchi wameshapoteza vitambulisho vyao kutokana na utunzaji mbaya hivyo kulazimika kwenda mamlaka  kuomba chengine wakati wenzao hawajapatiwa hata mara 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>