Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Matale hawana kituo cha afya

$
0
0
Na Hanifa Salim, Pemba
WANANCHI wa shehia ya Matale wilaya ya Chake Chake mkoa wa kusini Pemba, hawana kituo cha afya kwa miaka mingi sasa.

Walisema wamekuwa wakipata usumbufu wa kuitafuta huduma hiyo.

Mmmoja kati ya wananchi hao, Siasa Khamis Ali, alisema katika kijiji chao kituo cha afya ndio changamoto kubwa ambayo inawakabili na kwamba serikali inapaswa kulipatia ufumbuzi.

Nae Mkubwa Juma Abdalla, alisema tokea Mapinduzi ya mwaka 1964, hawajawahi kujengewa kituo cha afya.

Aliiomba serikali na viongozi wa ngazi za juu kuwaangalia kwa jicho la huruma ili kuhakikisha kituo cha afya kinajengwa.

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Hanuna Ibrahim Masuod, alisema tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi kwa ushirikiano na wananchi.


Msaidizi Sheha wa shehia ya Matale, Mwalimu Haji Mchande, aliiomba serikali na viongozi wa ngazi ya juu kusikia kilio chao cha muda mrefu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>