Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

OMANI NA UJERUMANI KUSAIDIA SEKTA YA HABARI ZANZIBAR

$
0
0


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na wana Habari kuhusu ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman ikiwa ni hatua ya kukuza mashirikiano ya Wizara yake na Nchi hizo. 
 Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Joseph Kilange akimkaribisha Waziri wa wizara hiyo azungumze na wandishi wa Habari kuhusu ziara yake yakikazi ya siku nane Nchini Ujerumani na Oman.

Na Rahma Khamis –ZJMMC.
Serikali ya Omani imeahidi kuisaidia Sekta ya Habari Zanzibar kwa kuliwezesha Gazeti la Zanzibar Leo kupata Mtambo wa kuchapishia Magazeti yake ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha nchi hiyo pia Imeahidi kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kwa kuliunganisha katika Mfumo wa Satalite ili liweze kusikiaka na kuonekana Duniani kote.
Waziri wa habari utalii,utamaduni , na michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuhusiana na mafanikio ya safari yake nchini Omani na Ujerumani.
Amesema kwa muda mrefu Gazeti la Zanzibar Leo linakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuchapishwa kwa gharama kubwa nje ya Zanzibar na hivyo kama Omani italeta Mtambo huo wa uchapishaji itasaidia sana maendeleo ya Gazeti hilo.
Kwa upande wa ZBC Waziri Mbarour amesema Omani italeta Gari mbili za kurushia mtangazo ya moja kwa moja na kufanya maboresho ya Studio za ZBC ili kuwa za kisasa zaidi.
Akizungumzia kuhusu Utalii, Waziri Mbarouk amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Utalii ya Omani watafanya matangazo ya pamoja ya kutangaza na kuimarisha Sekta ya Utalii katika nchi zao.

Ameongeza kuwa Omani itaruhusu ndege zake za Oman AIR kusafirisha watalii Wanaokuja Zanzibar kutoka nchi tofauti ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza Idadi ya Watalii nchini.
Kwa upande wa Ujerumani Waziri Mbarouk amesema nchi hiyo itaisaidia Zanzibar kupitia Chuo cha Habari cha Zanzibar kwa kuwapatia Vifaa vya kufundishia na kuboresha Mtaala wa Uandishi.
Aidha amefahamisha kuwa nchi hiyo pia itatuma Walimu kutoka Ujerumani ili kuja kufundisha masomo mbalimbali ikiwemo Lugha ya Kijerumani.

Katika Ziara hiyo ya kikazi ya Siku nane nchini Oman na Ujerumani Waziri wa Habari aliambatana na Viongozi waandamizi wa Wiazara yake ambapo waliweza kujadili na kuahidiwa misaada mbalimbali kutoka nchi hizo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>