Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ZSSF Yakabidhi Msaada wa Mabati kwa Ajili ya Kituo cha Afya Kinuni.

$
0
0
Jengo la Kituo cha Afya Kinuni kilichojengwa kwa Nguvu za Wananchi wa Shehia tatu za Kinuni, Mwera na Mtofaani, kikiwa katika hutua kubwa ya Ujenzi wake, Wanaomba msaada kwa swafadhili mbalimbali ili kuweza kutowa misaada yao kukamilisha uchenzi wake na kuwapunguzia mwendo wananchi swa maeneo hayo ambao hufuata huduma ya Afya ya Mama na Mtoto huduma hiyo mbali na maeneo hayo. juwa kituo hicho hakikukamilika ujenzi wake.Hutoa huduma ya Kliniki katika kjengo hilo kwa kinamama na Watoto katika sehemu hiyo ilioezekwa nusu mabati. Wanaomba msaada wenu Wadau wa Maendeleo ya Afya.     
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF) Ndg. Mussa Yussuf akimkabidhi mabati Sheha wa Shihia ya Mtofaani Bi Kijakazi Ferouz, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la kituo hicho kinuni Unguja.
 Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg.Mussa Yussuf, akizungumza na Wanakamati wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni wakati wa hafla ya kuabidhi mabati 150 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake kituo hicho kinahitaji mabati 187 ili kukamilisha ujenzi huo.
 Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni Ndg.Husein Ali akizungumzia ujenzi huo wakati wa kukabidhiwa mabati na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ili kuweza kuezeka kituo chao hicho na kuwataka Wananchi wengi kutowa msaada wao kuweza kumalizia ujenzi huo na kuaza kutowa huduma ya Afya kwa Wananchi swa Shehia hizo. Amesema kituo chao kitakuwa na sehemu ya Kliniki ya Watoto, Chumba cha kujifungulia Wazazi na kupata huduma nyengimu muhimu zinazotolewa kwa wananchi.Na kusisitiza kuwaomba Wananchi kuwapatia msaada ili kuweza kukimaliza kwa wakati muwafaka. 
 Sheha wa Shehia ya Mtofaani Bi. Kijakazi Ferouz, akitowa neno la shukrani kwa uongozi wa ZSSF kwa msaada wao wa mabati kukamilisha ujenzi huo wa kituo cha Afya Kinuni, ili kupunguza kero za wananchi wa maeneo hayo kufuata huduma ya afya mbali na makaazi yao, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo la kituo hicho huko kinuni.    
 Wanakamati wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kinuni wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg. Mussa Yussuf, akitowa maelezo ya Mfuko wa ZSSF, wakatri wa kukabidhi mabati 150 kwa ajili ya kuezekea kituo hicho cha Afya kilichojengwa kwa nguvu za Wananchi wa Shehia tatu za Kinuni. Mwera na Mtofaani kwa ajili ya kupata huduma za afya kituo hapo kupunguza mwendo wa kufuata huduma hizo mbali na makazi yao..   



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>