Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi wakanusha kupanga kuwafanyia kitu kibaya CHADEMA

$
0
0
Na Rose Chapewa, Mwanza
JESHI la polisi mkoani Mbeya limeelezea kusikitishwa na habari ya uchochezi  iliyoandikwa na  chombo kimoja cha habari, ikidai jeshi hilo litakifanyia kitu kibaya Chama cha Demokrasi na Mendeleo na kudai habari hizo zina lengo la kuligombanisha jeshi hilo na chama hicho.

Hayo yalibainishwa na Kamanda wa polisi mkoa huo, Ahmed Msangi,  wakati akizungumza na waandishi wa habari  na kuwashukuru kwa kufika  ofisini kwake kupata ufafanuzi na hivyo kuzingatia misingi na maadili ya uandishi ya kuandika habari sizoegemea upande mmoja, baada ya uongozi wa Chadema mkoa wa Mbeya, ukiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi, kulalamikia kauli hiyo.

Alisema habari hizo ni za uchochezi na zenye lengo la kuharibu uhusiano uliopo kati ya viongozi wa vyama vya siasa ikiwemo Chadema.

Alifafanua kuwa yeye ni kiongozi anayewatumikia wananchi wote na kwamba kiongozi yeyote mwenye maadili ya utumishi hawezi kusema kitu kama hicho huku akiwapa pole viongozi wa Chadema kwa habari hiyo ambayo imewaumiza.

“Hiyo habari nami pia nimeisoma kwenye gazeti, na baada ya kuiona nilimpigia simu mwandishi aliyeiandika na nikamwambia sijapenda kuandika kitu ambacho sikukisema, na pia hata bosi wake wa hapa Mbeya naye nilimweleza,” alisema.


Awali uongozi wa Chadema  mkoa wa Mbeya,  uliitisha mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, ukimtaka Kamanda Msangi, kukanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku la Kiswahili nchini, kuwa atakifanyia kitu kibaya chama hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, John Mwambigija, alisema kutokana na kauli hiyo chama kimejipanga kuhakikisha kinakabiliana na tatizo lolote litakalosababishwa na jeshi la polisi.

Alisema wanachama wa Chadema hawaliogopi jeshi la polisi, na kutoa siku tatu kwa kamanda wa polisi mkoa huo, kukanusha taarifa hizo.

“Sisi tuna taarifa za kiusalama kama wao wanavyosema tunapata taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, na tayari tumeshawaagiza vijana wetu, wanawajua polisi walioko uraiani, kama hatafuta kauli yake tutawaambia polisi walioko uraiani waende wakakae nyumba za polisi,” alisema.

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, alisema anasikitishwa na kauli ya kiongozi huyo aliyepewa dhamana na jeshi la polisi, na kumuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu, kumfuta kazi mara moja.


Alisema kauli hiyo ya vitisho si kwa ajili ya  wanachama wa Chadema tu bali inaathiri wananchi wote wa mkoa wa Mbeya, huku akijigamba kuwa  wakazi wote wa Mbeya ni wanachama wa Chadema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles