Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Polisi wajipanga kuwashughulikiwa wauza ‘unga’

$
0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, amekiri baadhi ya maeneo ya visiwa vya Zanzibar yanatumika kuingiza dawa za kulevya.

Alisema mwarubaini pekee  wa kukabiliana na tatizo hilo ni jamii  kuwafichua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo.

Alisema jamii inawatambua waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao na kuwataka kuondoa muhali kwa kutoa taarifa polisi ili wachukuliwe hatua.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kisiwani Pemba, alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa kupitia falsafa ya polisi jamii, bado uingizaji, usambazaji na utumiaji wa madawa hizo unaendelea.


Aidha alikiri baadhi ya maeneo katika kisiwa cha Pemba kuwa kitovu ya uingiaji wa dawa za kulevya na kuongeza kwamba wamejipanga kuyadhibiti maeneo yao hasa yenye bandari bubu kwa kuimarisha ulinzi na doria.

Aliwataka wananchi kuacha fikira hasi ya kwamba biashara ya dawa za kulevya ni hahali kwa kuwa inawapatia fedha.

Alisema vijana wengi ambao wamejiingiza katika wimbi la utumiaji wa dawa za kulevya wameishia jela kutokana na kushiriki uhalifu.


Maeneo ambayo yanaonekana kukithiri vitendo vya uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya katika mkoa wa kaskazini Pemba ni Mtambwe ambapo kuna bandari bubu nyingi na sheha ya Bopwe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>