Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Oman kulijengea uwezo ZBC

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Oman
OMAN imeahidi kuliimarisha Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) kwa kulipatia vifaa vitakavyoliwezesha kukusanya na kurusha matangazo yake na kuonekana vyema katika nchi za Mashariki ya Kati. 

Ahadi hiyo imetolewa mjini Muscat, Oman na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Redio na Televisheni za Umma wa Oman, Dk.Abdullah Bin Nasser Al Harrasi, wakati akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Said Ali Mbarouk akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini humo.

Alisema mamlaka yake ina dhima kuimarisha uwezo wa matangazo ya shirika hilo na kuonekana vyema Oman na kwengineko na hivyo iko tayari kulipatia vifaa vya kurushia matangazo kwa njia ya satellite  na matangazo ya moja kwa moja kwenye matukio nje ya studio.

Alisema hatua hiyo itazidisha kuimarisha uhusiano uliopo kwa vile itawawezesha wananchi wa Oman kuangalia vipindi vinavyorushwa na ZBC kwa wepesi zaidi kama ilivyo kwa matangazo ya redio na televisheni ya Oman yanavyopatikana Zanzibar.


Alisema kwa kuanzia kutakuwa na utaratibu wa kubadilishana mafundi na watayarishaji vipindi ili kuweka misingi ya kuandaa kwa pamoja vipindi vitakavyotumia lugha ya Kiswahili na Kiarabu na  kuwawezesha wananchi wa Oman na Afrika ya Mashariki kwa ujumla kufaidika na  matangazo ya vituo hivyo.

Akitoa shukrani kwa mamlaka hiyo, Waziri Mbarouk, alipongeza hatua hiyo inayokusudiwa kuchukuliwa na Oman na kusema sio tu itawawezesha wananchi wa pande hizo mbili kuendelea kuelewana zaidi na kupatiwa taarifa juu ya masuala mbali mbali lakini pia itasaidia kukuza na kuinua kiwango cha utalii katika nchi zote mbili.         


Waziri Mbarouk yuko Oman kwa ziara ya siku nne kutembelea vyombo vya habari, utamaduni na utalii na michezo kwa mwaliko wa serikali ya Oman kwa madhumuni ya kutafuta njia za kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>