Na Mwashamba Juma, Dar es Salaam
WAANDISHI wa habari nchini wameshauriwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kurahisisha kazi zao kwa kuziweka salama na kuzinusuru na athari za teknolojia hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari za magazeti ya Tanzania, Ofisa ruzuku wa Mfuko wa Vyombo vya habari Tanzania (MF), Dk. Dastan Kamanzi huko ukumbi wa ofisi hizo, Mhimbili jijini Dar es Salam wakati akiwapa taaluma ya kutumia mtandao wa “Google Drive” waandishi hao katika warsha ya ruzuku za vijijini.
Dk. Kamanzi alisema mtandao wa “google drive” ni kimbilio pekee kwa waandashi wa habari wasasa katika kuzinusuru kazi zao kuathiriwa na maendeleo ya teknolojia ikiwemo kuharibiwa na virusi kwenye komputa, kuibiwa ama kupotea.
Aidha alisema “goole drive” hurahisisha na kuepusha kutembea na “had ware” zikiwemo laptop, flash, recoders na asets nyengine kwa lengo la kuondosha usumbufu wa kubeba mizigo kila mahali.
“Ukiwa na “google drive” mwandishi huhitaji kuwa na matumizi ya ziada ya “flash disk,” CD au hardware yoyote hata ukiwa ya nje ya ofosi, hakuna ulazima wa kutembea na laptop kila mahala, simu yako ya mkononi inatosha hasa kwa waandishi wanaotoka nje ya mji” alifahamisha.
Alisifu uzuri wa taaluma ya “google drive” kwa kueleza kuwa hata mwandishi wa habari asipokuwa na huduma ya mtandao “internet”, bado anaweza kuhifadhi kazi zake na kuwa salama hadi wakati atakapokuwa nao nakuongeza kuwa kazi zake zitakuwa salama kwa ofisi na binafsi.
Mapema akiwasilisha mada ya “Uandishi wa makala”, msimamizi wa ruzuku za vjijijini katika warsha hiyo (Mentor), Burhan Khatib Muhunzi alisema bado kuna baadhi ya waandishi wa magazeti hadi sasa hawawezi kutofautisha baina ya makala na stori za kawaida katika uandishi wao.
Alisema makala lazima ifanyiwe utafiti wakina kabla ya kuandikwa kwake sambmba na kujitosheleza kuwa na vyanzo vingi vya habari vitakavyobeba wazo la stori husika sio mawazo ya mwandishi mwenyewe.
“Waandishi hakuna alisema kwenye makala wala huandiki mawazo yako, lazima ulifanyie utafiti wazo lako, muandike kilichozungumzwa chanzo chako cha habari, halafu uende ndani zaidi uibue yaliyojificha, ili umpe nafasi msomaji wako, sio alisema …alisema…” alifahamisha Mentor huyo.
Nae msimamizi Samson Kamalamo aliwataka waandishi hao kuzingatia maadili ya uandishi wahabari na kuongeza kwamba stori ilikuwa inamashaka na maadili, mwandishi anahaki ya kutoichapisha stori hiyo.
Kwa upande wa washiriki ambao ni waandishi wa habari za magazeti kutoka vyombo mbalimbali vya habari walikiri kwamba kuna baadhi ya vyombo vyahabari bado vinaendelea kukiuka maadili ya kiuandishi hususani mitandao ya jamii, zikiwemo globaz.
Walisema ni mwiko katika uandishi wa habari kuonesha sura za maiti ama watoto walidhalilishwa, lakini baadhi ya vyombo vya habari hufanya hivyo bila ya kutanguliza msamaha, hali ambayo inaitia dosari tathnia ya habari Tanzania.
Warsha hiyo ya wiki moja kwa waandishi wahabari za vijijini kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini imeandaliwa na kusimamiwa na Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania, TMF.