Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Teknolojia yasaidia kupunguza matumizi ya barua

$
0
0
Na Fatuma Kitima, Dar es Salaam

WIZARA ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, imeeleza kuwa kutokana na kuongezeka matumizi ya teknolojia duniani, uandishi wa barua umepungua miongoni mwa watu hasa vijana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, Katibu Mkuu Wizara hiyo, Prof. Patrick Makungu, alisema Umoja wa Posta Duniani, umeanzisha shindano la uandishi wa barua kwa wanafunzi katika skuli za msingi na sekondari.

“Niwapongeze walimu pamoja na wanafunzi katika skuli zote zilizoshiriki kwa mwaka huu kwani ni chachu kwa vijana wetu kuelewa namna sahihi ya uandishi wa barua jambo ambalo ni mahitaji ya msingi katika mawasiliano rasmi na maisha ya utendaji kazi wa kila siku,” alisema.



Aliwapongeza washindi walioshiriki katika shindano hilo ambapo msindi wa kwanza atawakilisha Tanzania katika shindano hilo duniani.

Aliwataja washindi hao kuwa ni Glory Mduma ambaye ni mshindi wa kwanza kutoka skuli sekondari ya St.Mary, mshindi wa pili Ndehovye Nyindo kutoka skuli ya sekondari Kifungilo ya Wanawake na wa tatu Khadija Yassin kutoka skuli ya St.Mary Mazinde Juu.

Alisema utoaji wa huduma ya posta unapaswa kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano na kuhakikisha huduma hizo zinaimarishwa.

Alisema katika kuimarisha mabadiliko hayo serikali imeanzisha mchakato wa uhusishaji wa sera ya taifa ya Posta ili kupata sera mpya itakayohusisha mazingira mapya ya utoaji wa huduma za posta,usalma wa barua na vifurushi,ushindani na maendeleo ya teknolojia.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma, alisema huduma ya posta imekuwa na taswira tofauti kwa wananchi hasa baada ya ujio wa tekonolojia ya mawasiliano.

Kwa upande wa wanafunzi walioshinda katika shindano la uandishi wa barua, mshindi wa kwanza, Glory Mduma, kutoka skuli ya sekondari St.Mary, alisema amefurahi kupata ushindi huo na kuwaomba wanafunzi wenzake kushiriki mashindano yajayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>