Na Laylat Khalfan
Ngombe na Mbuzi wapatao 201 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa viwele baada ya kufanya uchunguzi katika kipindi cha kuanzia Januadi hadi Septemba mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mtaalamu wa kufuatilia magonjwa ya wanyama na huduma za maabara, Waridi Abdalla Mussa, alisema, ugonjwa huo umewaathiri zaidi ng’ombe.
Alisema ugonjwa huo umegundulika wilaya zote za Unguja na wilaya za Chake Chake na Wete kwa Pemba.
Aliwataka wafugaji hao kuhakikisha wanaipatia kinga mifugo yao dhidi ya maradhi ya kuambukiza.
Alisema ugonjwa huo husababishwa na bektiria, virusi na fangasi ambapo vimelea hivyo vinawashambulia wanyama hao kwa sabababu ya kuwekwa kwenye mazingira yasiyostahiki.
Magonjwa mengine yanayowaathiri wanyama hao ni chambavu, maradhi ya ngozi,nimonia na maradhi ya vibuma ambayo husambazwa na kupe na inaaminika kuwa huathiri ng’ombe kwa zaidi ya asilimia 89 na huua idadi kubwa ya ndama.
Aliwashauri wafugaji kuwapeleka wanyama wao kliniki kwa ajili ya kupatiwa chanjo ili kuweza kuondokana na magonjwa hayo.