Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ulinzi baharini wakabiliwa na changamoto

$
0
0
Na Hafsa Golo
Licha ya serikali kujipanga  kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya ukanda wa bahari,bado kumekuwa kukijitokeza changamoto  mbali mbali kunakosababishwa na upungufu wa vitendea kazi.
Hali hiyo imesababisha bidhaa za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya kuiendelea.

Kamanda wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo, Luteni Hussein Ali Makame, alisema maeneo ya bahari mara nyingi hutumiwa na maharamia pamoja na watu ambao wanajishughulisha na biashara haramu kuvushia bidhaa zao.

Alisema kikosi hicho katika doria zake kimekamata vyombo vidogo venye silaha na mabomu na  boti moja ndogo yenye mashine na vifaa vya matumizi ambayo ilisadikiwa ni ya maharamia.

Aidha alisema tukio jengine walilolibaini katika doria zao ni wavuvi wa kigeni kutumiwa bahari ya Zanzibar kwa  shughuli za uvuvi haramu.

“Tuliwahi kukamata boti namba 9 ya Maputo Msumbiji ikifanya uvuvi bila kufuata sheria,” alisema.
“Zanzibar ni visiwa na siku zote doria zinatakiwa kufanywa lakini kukosekana nyezo za kisasa za doria kunasababisha shughuli za doria kukwama,” alisema.

Meja Jenerali Rogastian Shabani Laswari wa jeshi la Wananchi Tanzania,ambae pia ni Kamanda wa kikosi cha majini,  alisema eneo la bahari  ni kubwa hivyo linahitaji doria za mara kwa mara  jambo ambalo limekuwa changamoto kutokana na uhaba wa vitendea kazi.
Alisema kutokana na changamoto hizo, itakuwa vigumu kuzuia kwa asilimia 100, kuwadhibiti wakorofi kutumia bahari hiyo kwa shughuli zao.
Hata hivyo, alisema suala la usalama kwa jumla linaridhisha licha ya kuwepo changamoto kadhaa.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar, alikiri kuwepo kwa changamoto katika usafiri wa bahari hususan maeneo ya bandari bububu ambapo zimekuwa zikitumika katika usafirishaji wa biashara haramu kwa lengo la kukwepa kodi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>