Balozi Seif akihutubia waumini wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Peramiho alipofanya ziara fupi na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti huo.kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambae pia Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kepteni Aseri Msanga na sheikh Mkuu wa Kijiji cha Peramiho Sheikh Said Rasid, wakati kushoto yake balozi ni mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Kikundi cha dhikri cha Msikiti mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Peramiho Mkoani Ruvuma kikimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani kukagua ujenzi wa msikiti wao.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Peramiho wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani wakati alipote mbelea harakati za ujenzi wa msikiti wao wa ijumaa wa Masjid Jidah.
Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake akikagua ujenzi wa msikiti wa ijumaa wa kijiji cha Peramiho wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Ruvuma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Peramiho { Masjid Jidah } mara baada ya kuwahutubia waumini wa msikiti huo.(Picha na Hassan Issa– OMPR)