Mkurugenzi wa miradi ya Jamii ya TASAF, Tanzania Amadeus Kamagenge, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waalimu, madaktari na wasimamizi wa miradi ya mfuko huo, kwa walengwa kutoka shehia zilizomo kwenye mpango, yaliofanyika chuo cha Amali Chakechake, Pemba, kulia ni meneja wa uhaulishaji fedha Omari Malilo, na kushoto ni kaimu Afisa mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais Pemba Khadija Khamis Rajab akifutaiwa na afisa mdhamini fedha Bakar Haji.
Afisa habari wa TASAF makao makuu Dar- es Saalam Zuhura Mdungi akiwasilisha mada namna ya kujaza fomu za malalamiko kutoka kwa wananchi walengwa, mafunzo hayo yaliwahusisha waalimu, madaktari na wasimamizi ya miradi hiyo kwenye shehia zilizomo kwenye mpango kisiwani Pemba
Washiriki wa mafunzo ya siku mbili juu ya ujazaji fomu maalumu kwa kaya lengwa, ambazo zinawezeshwa na TASAF, wakimsikiliza Afisa Habari wa TASAF Zuhura Mdungi, wakati akiwasilisha mada juu ya namna ya kuwasilisha malalamiko na kujaza kwenye fomu husika, mafunzo hayo yalifanyika jana Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba
Kaimu Afisa Mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais Pemba Khadija Khamis Rajab, akifunga mafunzo kwa waalimu, madaktari na wasimamizi wa miradi inayowezeshwa na TASAF kwenye kaya lengwa, mafunzo hayo yalifanyika chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba(Picha na Haji Nassor Pemba)