Meneja Mradi wa huduma kamilifu kwa kinamama baada ya kuharibika kwa mimba Ngitoria Lemonduli akielezea malengo ya mradi huo mpya uliozinduliwa katika ukumbi wa Hoteli ya Mazsons Shangani, Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Haji Mwita Haji akizindua Mradi mpya wa huduma kamilifu baada ya mimba kuharibika katika Hoteli ya Mazsons Shangani,
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Marie Stopes Tanzania ambae ni Mkurugenzi Rasilimali watu na Utawala Bi Elly Reweta akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi na kufunga mafunzo kwa wahudumu wa Afya Zanzibar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi huo Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar Dkt. Haji Mwita Haji akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya wiki mbili ya huduma kamilifu baada ya kuharibika kwa mimba ambayo yalidhaminiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Marie Stopes Tanzania.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Dkta Haji Mwita Haji akizungumza na washiriki wa mafunzo na wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi wa huduma kamilifu baada ya mimba kuharibika.
Baadhi ya waalikwa na washiriki wa mafunzo ya wiki mbili ya huduma za akinamama baada ya kuharibika kwa mimba wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo.
Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa shukrani kwa Shirika la Marie Stopes baada ya kudhamini mafunzo ya wiki mbili ya kuwajengea uwezo watoa huduma ya afya 20 wa mradi wa huduma kamilifu kwa kinamama baada ya kuharibika kwa mimba.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo)