Na Zuhura Juma, Pemba
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, ameitaka Wizara ya Kilimo kuongeza bidii ya kuotesha miche ya mikarafuu na kuigawa kwa wakulima.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Wete, alisema wananchi katika mkoa wake sasa wamehamasika kupanda mikarafuu kwa wingi, ili kujipatia maendeleo.
Alisema kwa vile wananchi wamehamasika na kilimo hicho, hakuna budi wizara kuongeza bidii ya kupanda miche ili kuwahamasisha zaidi wakulima hao.
Alisema uchumi katika mkoa huo umekua, kwani wananchi wamekubali kujituma katika njanja tofauti ikiwemo kilimo kwa upanda mazao ya biashara na mbogamboga.
Akizungumzia amani na utulivu katika mkoa wake, alisema inardhisha na kusema atahakikisha inadumishwa.