Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Changamoto za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

$
0
0
Na Kauthar Abdalla

WIZARA ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imeandaa mkakati wa utekelezaji itifaki ya soko la pamoja ili kurahisisha na kuondoa changamoto zinazolikabili soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkakati huo unatoa muelekeo wa utekelezaji wa soko la pamoja katika ngazi ya kitaifa kwa kuendeleza muundo, mipango ya kisekta na programu zitakazosaidia ukuaji wa uchumi.

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora, Salum Maulid Salum, katika ufunguzi wa warsha ya kujadili rasimu ya mkakati wa utekelezaji wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyofanyika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Alisema dhamira ya mkakati huo ni pamoja na kuziainisha changamoto na fursa za soko la pamoja,kuonesha uwezo na upungufu wa Watanzania katika kuchangamkia fursa za soko hilo.

Pia alisema dhamira nyengine ni kuainisha mbinu za kupambana na changamoto, nafasi za taasisi za serikali katika utekelezaji wa soko hilo na kutoa muongozo wa kimkakati katika kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya soko hilo.

Aidha alisema utekelezaji wa mkakati huo utasaidia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza fursa za biashara na uzalishaji,kupanua soko la bidhaa za kilimo na viwanda,kutoa fursa kwa wawekezaji na kuwasaidia Watanzania kupata ajira.

Hata hivyo, alisema utekelezaji wa itifaki ya soko hilo umeanza rasmi 2010 leo ilikiwa ni kuimarisha ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa kurahisisha mzunguko huru wa bidhaa, watu, wafanyakazi, huduma na mitaji ndani ya nchi wanachama.

Mkurugenzi Msaidizi idara biashara, uwekezaji na sekta za uzalishaji  Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki, Dk. Abdul Makame, alisema  nchi wanachama zinatambua umuhimu wa sekta binafsi na kuzipa kipaombele.


Alisema itifaki ya soko la pamoja inaangalia zaidi uchumi huru wa mitaji ya wanachama ili kuhakikisha lengo linafikiwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>