Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Miradi ya dola 236m yasajiliwa ZIPA

$
0
0
Na Mwanajuma Mmanga

Jumla ya miradi 19 yenye thamani  ya dola za Marekani  236 milioni imewekezwa  kuanzia Januari hadi Oktoba 2014.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uimarishaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor, alisema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maruhubi.

Alisema miradi hiyo ni pamoja na ya sekta ya biashara, hoteli ya mikahawa, huduma, afya na  utembezaji wageni na michezo ya baharini.

Alisema katika sekta ya biashara miradi miwili yenye thamani ya dola 22,319,758 imesajiliwa, hoteli na mikahawa miradi 7 yenye thamani ya dola 52,031,235 na huduma miradi 6 yenye thamani ya dola 160,780,000.

Miradi mengine ni ya  afya mradi mmoja wenye thamani ya dola 1,275,000 na mradi mmoja wa watembeza wageni na michezo ya baharini wenye thamani ya dola 500,000.


Alisema miradi hiyo imeanzishwa kutokana na Zanzibar kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji yanayowavutia wawekezaji wengi.

Alisema majukumu ya ZIPA ni pamoja na kurahisisha na kuwasaidia wawekezaji kupata vibali, kuwaunganisha, kutafuta taarifa kwa ajili ya wawekezaji na wafanyabishara na kutatua changamoto zinazojitokeza katika uwekezaji.


Aliwataka wawekezaji kufuata masharti na taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>