Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

WHO kuimarisha huduma za afya

$
0
0
Na Fatma Kassim
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Rashid Seif Suleiman, amesema Zanzibar inafaidika na misaada mbalimbali inayotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika kupambana na vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Akifungua mkutano wa wafanyakazi wa WHO nchini Tanzania katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort,alisema misaada hiyo inatokana na programu mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangia kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito.

Alisema kwa muda mrefu Zanzibar ilikuwa inakabiliwa na matatizo mbali mbali lakini kupatikana kwa ofisi ya kudumu na wataalamu wa shirika hilo nchini,matatizo hayo yamepungua.

Alilifahamisha shirika hilo kamba Zanzibar imechukua hatua madhubuti kuzuia kuingia ugonjwa wa ebola kwa kuweka udhibiti na upimbaji wa watu katika mipaka ya kuingilia nchini.

Mwakilishi Mkaazi wa WHO, Rofaro Chatora, alisema mkutano huo una lengo la kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa kazi sambamba na kupanga mikakati 
mipya ya kuimarisha ufanisi wa kazi zao.


Alisema kwa mwaka 2015 wanakusudia kuisaidia Zanzibar kifedha katika kutekeleza sera zake za kuimarisha afya ikiwemo kuwapatia mafunzo wafanyakazi, kuimarisha utafiti katika 
masuala ya afya.

Mambo mengine ni kufuatilia hali ya maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza sambamba na kuwajenga uwezo wataalamu wa afya wa Zanzibar kwa lengo la kuongeza ushirikiano wa kimataifa.


WHO limekuwa likiisaidia Zanzibar katika harakati za kupambana na maradhi mbali mbali ikiwemo UKIMWI, kifua kikuu, malaria na afya ya mama na mtoto ambapo katika mkutano huo wa siku nne wafanyakazi wa WHO waliopo Tanzania watajadili mambo mbalimbali ya kuongeza ufanisi wa kazi zao. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>