Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Madeni watumishi wa umma kumalizwa Disemba

$
0
0
Na Fatina Mathias, Dodoma
Serekali imesema itamaliza kulipa madeni ya watumishi wa umma kiasi cha shilingi bilioni nane mwezi Novemba na Disemba mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah  Salum, aliyetaka kujua kwa nini serikali inakuwa na malimbikizo ya watumishi ya muda mrefu.

Alisema mpaka sasa serikali inadaiwa shilingi bilioni 8 kwa upande wa watumishi wa umma na itahakikisha inalipa kuanzia Novemba na Disemba.

Alibainisha kwa watumishi wa mambo ya ndani ya nchi wanadai kiasi cha shilingi milioni 800.


Alisema wakati mwingine hali ya malimbikizo hayo yanatokana na baadhi ya watumishi wapya kuchelewa kupitia kazini pindi wanapoajiriwa.

“Kwa utaratibu uliopo hivi sasa,mtumishi anapoajiriwa na kuwahi kuripoti kazini,mwisho wa mwezi anapata mshahara wake isipokuwa kwa wake wanaochelewa kuripoti,”alisema.


Alisema sasa mtumishi anayeajiriwa na kuripoti kazini kuanzia tarehe moja hadi 10, mwisho wa mwezi anapata mshahara wake kama kawaida, na wanaoripoti baada ya tarehe 10, wanaweza kukosa mshahara wa mwezi husika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>