Na Hafsa Golo
Wachimba makaburi Mwanakwerekwe, wameiomba serikali na waumini wa dini kulipatia hifadhi eneo hilo ili kudhibiti vitendo vya kishirikina vinavyoendelea kufanya katika eneo hkithiri katika eneo hilo.
Walisema hayo kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na Zanzibar Leo.
Walisema njia muafaka ya kuvidhibiti vitendo hivyo ni kumalizwa ujenzi wa uzio uliosita kwa muda mrefu sasa.
Mchimba makaburi aliejitambulisha kwa jina la Mohamed Nassour Juma (51) alisema, makaburi yamekuwa yakifukuliwa na kuzikwa vitu mbali mbali vya kishirikina ikiwemo vyungu,samaki waliofungwa kama sanda, mayai na nazi.
Aidha alisema pamoja na jitihada wanazochukua kuzuia vitendo hivyo, bado vimekuwa vikiendelea.
Alisema wakati wakichimba makaburi wamekuwa wakikuta ndege ambao wamezikwa kama binaadamu.
Mchimbaji makaburi mwengine, Aboud Jumbe Askar (29) alisema wamechoshwa na vitendo vya kishirikiana vinavyofanywa hususan ndani ya makaburi.
Mkaazi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Asha alikiri makaburi kutumiwa kwa imani za kishirikiana ambapo mwanzo walikuwa na hofu lakini hofu hiyo sasa imeondoka.
Aliishauri viongozi wa siasa,wakiwemo Wabunge na Wawakilishi kutafuta njia mbadala kuhakikisha uzio wa eneo hilo unamalizika ili kupunguza vitendo hivyo.