Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Walioathirika mafunzo JWTZ Unguja Ukuu kufidiwa

$
0
0
Na Augusta Njoji, Dodoma
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, zitafanya uchunguzi wa matukio ya kulenga shabaha katika eneo la Unguja Ukuu yaliyofanywa na JWTZ Zanzibar  kama yamesabanisha  madhara na ikibainika kuna walioathirika watalipwa fidia.

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hussein Mwinyi, alisema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub.

Katika swali lake Jaku alitaka kujua kama serikali ipo tayari kutoa fidia kwa madhara yanayotokea na yatakayotokea kwa wananchi wa Unguja Ukuu na wale ambao tayari wameathirika.

Pia alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kubadilisha matumizi ya eneo hilo haraka ili kunusuru uwezekano wa kutokea  vifo na majeruhi kwa wananchi wa maeneo hayo.


Akijibu maswali hayo, Dk. Mwinyi, alisema mazoezi ya kijeshi ndio msingi mkuu wa utendaji kivita katika majeshi yote duniani likiwemo Jeshi la Ulinzi ka Wananchi wa Tanzania hivyo hayana budi kufanyika.


Alisema kwa sasa jeshi halina eneo mbadala la kufanyia mazoezi ya kijeshi kisiwani Unguja kwa kuwa hakuna maeneo mengine makubwa yanayoweza kutumika kwa majukumu hayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>