Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Z’bar kuanza kuzalisha mishumaa

$
0
0
Na Meibaku Mollel, TSJ Pemba
Uongozi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo na arki ya mimea kisiwani Pemba, unatarajia kuanza kuzalisha bidhaa mbali mbali zenye ubora, kwa kushirkiana na kampuni ya Land ya Japan, kuanzia mwezi Disemba mwaka huu, ikiwa ni pamoja na mishumaa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini kwake, Meneja wa kiwanda hicho, Ramadhani Kombo Ferouz, alisema uzalishaji wa bidhaa hizo ambazo baadae zitawekwa nembo maalumu, umekuja kutokana na kuendelea kuwepo ushirikiano na kampuni hiyo.

Alisema wameamua kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na kampuni hiyo, ili k kutengeneza bidhaa zilizoongezewa ubora wa hali ya juu, ambazo zitakitangaza kiwanda hicho.

Alisema bidhaa wanazotarajia kuzalisha mwezi ujao, zitauzwa ndani na nje ya Zanzibar na zitakuwa na nembo yenye jina la Zanzibar Valore.


Alisema uzalishaji bado haujanza isipokuwa wametengeneza baadhi ya vifaa kwa ajili ya kufanya maonesho ya awali ya bidhaa wanazotarajia kuzalisha kwa ushirikiano na kampuni hiyo.


Alisema wataalamu kutoka Japan watawasili Zanzibar mwanzoni mwa mwezi ujao kwa ajili matayarisho ya uzalishaji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>