Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wakulima wapatiwa mashine kuzalisha mafuta ya alizeti

$
0
0
Na Tatu Makame
Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar, imetumia jumla ya shilingi 25 milioni kununulia mashine ya kuchujia mafuta ya alizeti, itakayowanufaisha wananchi wa maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Unguja.

Mashne hiyo ina uwezo wa kusafisha mafuta dumu 100 za ujazo wa lita 20 kwa siku, mafuta ambayo hayana aina yoyote ya kemikali.

Akizindua mashine hiyo katika kijiji cha Bambi wilaya ya kati Unguja, Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar,Dk. Sira Ubwa Mamboya,alisema kuwepo kwa mashine hiyo kutasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Aidha alisema,kuna vijana wengi wanaosubiri ajira kutoka serikalini,hivyo mashne hiyo itasaidia kupunguza dhana hiyo kwani vijana wataweza kujiajiri.

“Kuna vijana wengi wanaosubiri ajira kutoka serikalini, hivyo kuwepo kwa mashine hiyo kutasaidia kupungua tatizo la ajira kwa vijana,” alisema.

Alisema huu ni wakati mzuri wa kubadilisha maisha ingawa Zanzibar ni nchi ndogo lakini endapo wananchi watabadilika kuna uwezekano mkubwa wa kupata maendeleo.

Nae  Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti kutoka wizara hiyo, Mariam Juma Abdalla, alisema,wizara  imechukua juhudi za  kuwawezesha wakulima ili kuondokana na umaskini.

Aidha alisema mabwana na mabibi shamba 80 Unguja na Pemba wamepewa elimu ya kuwafundisha wakulima jinsi ya kutumia mashine hizo.


Alisema wizara imo kwenye mchakato kwa kutafuta mashine nyengine ili na wakulima wa kisiwa cha Pemba na wao wafaidike,
Nao wakulima wa zao hilo, walisema watahakikisha mashine waliyopewa wanaitumia ipasavyo ili kuendeleza kilimo cha alizeti.


Usssi Yahya akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake waliiomba  serikali kuwapatia maeneo yanayoweza kuzalisha alizeti ili kuinua uchumi wa nchi kwani mafuta ya elizeti yana soko kubwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>