Afisa mwongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bi. Mossy Kitangita (kulia) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka namna kitengo cha uongozaji wa ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kinavyofanya kazi na changamoto wanazokabiliana nazo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akimuuliza swali Bw. Nyello Abeid, mkufunzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini kuhusu alipotembelea banda la maonesho la chuo hicho leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini.
Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. John Mayunga akifafanua utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika usafiri wa anga.
Mkuu wa masuala ya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Ole Laputi (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la maonesho la idara hiyo kuhusu baadhi ya vimiminika visivyoruhusiwa kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka (Kushoto) akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuona utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu na viwanja vya ndege katika maeneo mbalimbali nchiniPicha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani yanayoendelea nchini na namna Serikali kupitia Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ilivyojipanga kuhakikisha usalama wa ndege na abiria wanaotumia anga la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).