Mdau barabara ya mombasa kwenda kiembesamaki ikiwa katika hali ya harakati za magari wakati wote kama inavyoonekana pichani ikiwa katika hali hiyo. Tafauti na miaka ya nyuma katika miaka ya 80 barabara hii ilikuwa kumuona mtu au gari ni nadra kutokana na hali ya kusema huku shamba kila mtu hakutaki kuwa makaazi yake tafauti na sasa eneo hili limekuwa mali na viwanja kuwa bei ya juu na majengo yake. Hii ni moja ya maendeleo ya kupanua miji sio kukaa eneo moja la mjini kila sehemu inaweza kuwa mji kama utakuwa na maendeleo kama ulivyo mji huu.
Na sasa mji wa tunguu kila mtu anaona bado ni shamba laki itafika wakati sehemu hiyo itakuwa mali na viwanja vyake kufikia bewi ya juu. Kila mtu atataka sehemu hii wakati sasa kila mtu anakupuuza na kudharau eneo hilo.