Na Mwandishi wetu, Dar
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kazi ya uchukuaji alama za vidole, picha na saini za kielektroniki kwa waombaji wa vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu wapatao milioni 2,900,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo.Zoezi hili lilianza Julai 15 katika wilaya ya Temeke ambayo imegawanywa katika kanda tano, itafuatiwa na wilaya ya Ilala na kuhitimishwa Kinondoni.
Taarifa ya NIDA imesema kila wilaya imegawanywa katika kanda, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri na kurahisisha zoezi kwa kuwapunguzia usumbufu wa kukaa muda mrefu kusubiri.
Zoezi la uchukuaji alama za vidole linakwenda sambamba na ujazaji fomu kwa waombaji wapya ambao hawakupa fursa ya kujaza fomu wakati wa zoezi la ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa.
Taarifa hiyo imewaomba wanahabari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu vitambulisho vya Taifa.
Imesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na hayo ni matunda ya wanahabari nchini kote.