Mwenyekiti wa Mkutano wa kutoa Maoni ya Katiba Mpya Tanzania Jasadi A Bungala, akiendesha Kikao cha kutowa maoni ya Katiba Mpya kupitia Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Unguja kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni.
Wajumbe wa Mkutano wa kutoa Maoni kupitia Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Unguja wakiwa katika mkutano huo wa kuwasilisha maoni yao kuhusu katiba mpya, iliowashirikisha Watu wenye Ulemavu Unguja, ulioandaliwa na Kituo cha Masuala ya Ulemavu na Maendeleo Jumuishi.
Wajumbe wa mkutano wa kutoa maoni ya Katiba Mpya kupitia Jumuiya ya Walemavu Zanzibar wakimsikiliza mtoa mada katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi mnazimmoja.
Mkurugenzi wa Idara ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar. Abeda Rashid Abdalla, akichangia na kutowa maoni yake katika mkutano wa maoni ya Katiba Mpya, uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi lazamani Mnazi mmoja.
Mwanachama wa Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Unguja akichangia vipengele vya kumuwezesha Mtu Mwenye ulemavu kuwekwa katika Katiba Mpya wakati wa kuchangia maoni ya Katiba Mpya kwa jumuiya hiyi.