Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Ma RC,DC Wapendekeza Serekali Mbili.

$
0
0
Na Fatma Kitima, DSM
WAKUU wa Mikoa na Wilaya nchini wanapendekeza msingi mkuu wa kudai haki kwenye katiba mpya utanguliwe na wajibu ili Watanzania wajenge utamaduni wa kuwajibika ambao utakuwa ni kichocheo cha maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema maoni yao kuhusu rasimu ya katiba ni juu ya muundo wa serikali, masuala ya kisheria, tunu na alama za taifa pamoja na wajibu na haki za raia.

Alisema kuhusu muundo wa serikali baraza lao la katiba linapendekeza serikali mbili kama ilivyo sasa.

Alisema sababu za baraza hilo kupendekeza serikali mbili ni kutokana na kuona kuwa kuwepo kwa serikali tatu kutakuwa na kila dalili ya rasilimali zinazotegemewa kuendesha serikali zote tatu zinazopendekezwa na hivyo kuuweka muungano katika hali tete.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni nchi inaweza kuingia kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba endapo vyama tofauti vya siasa vitashinda uchaguzi kwenye kiti cha urais.

Hata hivyo, aliongeza kuwa tafiti zinaonesha kuwa kuwepo kwa serikali tatu kuna uwezekano wa kuvunjika Muungano.

Kandoro alisema, wanapendekeza katiba mpya itambue tunu ya amani na utulivu kuwa ni moja ya tunu na alama za taifa kwa kuwa amani na utulivu ndiyo msingi mkuu wa shughuli zote binafsi na za pamoja katika kufikia malengo yoyote kimaendeleo.

Kuhusu masuala ya uraia yanayowagusa wananchi moja kwa moja na rasilimali zao, ameshauri katiba mpya itoe maelekezo ya wazi ili Mtanzania awe ni mtu anayejipambanua kwa sifa za wazi badala ya sifa zinazopendekezwa kwenye rasimu ya katiba.

Alisema baraza hilo pia linapendekeza kuongezwa kipengele cha kudumisha na kuhakikisha rasilimali za nchi zinamilikiwa na Watanzania.

Baraza hilo limeafiki masuala ya mgombea huru pamoja na Mawaziri kutotokana na Wabunge.

Kuhusu kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kandoro alisema sharti la kuzaliwa la mgombea wa kiti hicho kwenye katiba mpya lisomeke kuwa awe ni raia wa kuzaliwa kwa baba na mama.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amewataka Watanzania kuipitia rasimu ya katiba kwa makini na kutoa maoni juu ya mambo mbalimbali yaliyomo kwenye rasimu hiyo badala ya kujadili zaidi suala la nafasi ya urais na muundo wa serikali peke yake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>