Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hatma ya Dhamana ya Shekh. Ponda Septemba 17

$
0
0
Na Rose Chapewa
HATMA ya dhamana na Katibu wa Taasisi za Jumuiya ya Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda sasa itajulikana Septemba 17.

Sheikh Ponda alifikishwa tena mahakamani jana mjini Morogoro chini ya ulinzi mkali wa askari magereza na polisi waliokuwa na silaha.

Wakili wa serikali Bernard Kongola alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Richard Kabate, kwamba mshitakiwa anakabiliwa na mashtaka makubwa na hapaswi kupewa dhamana.

Upande wa mashtaka unadai Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu na hapaswi kupewa dhamana kwani anaweza kuhatarisha amani.

Shitaka la kwanza linalomkabili linadaiwa kutokea Agosti 10 katika eneo la kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro, ambapo aliwambia Waislamu wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

Alidaiwa kuwambia Waislamu hao kuwa kama watajitokeza kwao watu hao na wakajitambulisha kwamba wao ni kamati za ulinzi na usalama za misikiti, wafuge milango na madirisha ya msikiti na wawapige, kauli ambayo Mwendesha mashtaka anadai iliumiza imani za watu wengine.

Alidai kosa hilo ni kinyume cha agizo la mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam iliyotolewa na hakimu V. Nongwa, Mei 9 mwaka huu ambayo ilimtaka ndani ya mwaka mmoja ahubiri amani na asijishughulishe na uvunjifu wa amani.

Katika shitaka la pili wakili huyo alidai kuwa Agosti 10 mwaka huu katika eneo la kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro na mkoa wa Morogoro, mshitakiwa alitoa maneno yanye nia ya kuumiza imani nyingine za dini kwa kuwaambia Waislamu kwamba serikali ilipeleka wanajeshi

Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua,kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu, lakini serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa

Loliondo walipokataa mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakaazi wake ni Wakristu.

Mwanasheria huyo alidai maneno hayo yaliumiza imani za watu wengine na kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria 129 cha mwaka 2002.

Pia katika shitaka la tatu ilidaiwa Agosti 10 mwaka, huu eneo la kiwanja cha ndege manispaa na

ya Morogoro, mshitakiwa aliwashawishi Waislamu kujumuika kinyume na sheria na kuwaambia kuwa serikali ilipeleka jeshi Mtwara

kushughulikia suala la vurugu uliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Waislamu

lakini serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipotaka mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo na kudai ni maneno yaliyoashiria uvunjifu wa amani kinyume na kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kukana hakimu Kabate alimpa nafasi mshitakiwa, ambapo alisema anakubali tarehe ya mkutano ambayo ni
Agosti 18 mwaka huu, tarehe ya kukamatwa akiwa jijini Dar es Salaam Agosti 11 na jina lake.

Mshitakiwa lipotakiwa kusaini maelezo hayo wakili wake Juma Nassor alidai mahakamani kuwa hawezi kwa kuwa anatumia mkono wa kulia ambao alipigwa risasi hivyo mahakama ikubali kusaini kwa kutumia dole gumba la mkono wa kulia.

Aidha upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, ulidai upepelezi umekamilika na utapeleka vielelezo mbalimbali, ikiwemo DVD, kibali cha mkutano, hukumu no 245/2012 iliyotolewa na hakimu

Nongwe pamoja na mashahidi 15 kwa ajili ya kuthibitisha shitaka na kuomba tarehe ya kusikilizwa shauri hilo.

Hata hivyo, wakili wa utetezi aliiomba mahakama impatie dhamana mteja wake katika mashitaka yote matatu aliyoshitakiwa, pamoja na maelezo ya mlalamikaji kwa ajili ya kuandaa utetezi.

Wakili wa serikali alidai ombi la dhamana halina msingi, kwa kuwa tayari walishawasilisha nakala ya cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka inayopinga dhamana kwa mshitakiwa.

Alifafanua kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka anayo mamlaka ya kupinga dhamana kwa kutoa cheti, na alikubali ombi la kumpa maelezo mlalamikaji.

Maelezo hayo yalipingwa na wakili wa utetezi na kudai kuwa karatasi hiyo haina mahali inapoonesha imetumwa mahakamani, wala mahali panapooonesha afisa wa mahakama kupokea ili iingizwe kwenye jalada na kwamba katika katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 13, ibara ndogo ya 6 B inamtambua mteja wake ni mtu asiye na hatia hadi itakapothibitishwa na mahakama, hivyo ana haki kupewa dhamana.

Kwa upande wake Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba Septemba 17 ili kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya mshitakiwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>