Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Sultan Qaboos Aipa Zanzibar 12bn/-. 16 Wadhaminiwa na Masomo ya Juu Kupitia Qaboos Fund.

$
0
0
Na Kassim Ali, Amina Abeid, ZJMMC
SULTAN Qaboos bin Said wa Oman ametoa msaada wa riali 3,100,000 (zaidi ya shilingi bilioni 12.669) kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa katika eneo la Chuo cha Kiislamu Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna alisema ujenzi wa msikiti huo unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kutiwa saini makubaliano ya msingi kati ya Zanzibar na Oman.

Alisema msikiti huo, pamoja na shughuli za ibada, pia utakuwa ni chimbuko la kuanzishwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Zanzibar na kufanikisha azma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume aliependekeza kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu katika eneo hilo wakati akikifungua chuo hicho.

“Maandalizi yote ya ujenzi msikiti huu yamekamilika na utakuwa na sehemu ya kusalia wanawake na wanaume, madarasa sita ya kusomea, chumba cha kompyuta na maktaba ya kisasa,” alisema.

Akizungumzia msaada wa masomo ya elimu ya juu uliotolewa na Mfalme Qaboos kupitia mfuko wa Sultan Qaboos Academic Fellowship, alisema umeanza kuleta mafanikio na wanafunzi wa kwanza 16 wataanza kufaidika na msaada huo mwaka huu.

Alisema wanafunzi tisa watasoma shahada ya uzamivu (PhD) na saba watachukua shahada ya uzamili katika fani walizoomba na watajiunga kwenye vyuo vikuu vya nchi tofauti duniani.

Aliongeza kuwa awali Wazanzibari 170 walipeleka maombi ya kupatiwa nafasi hizo kupitia mtandao na baada ya mchakato uliofanywa na kamati mbili zilizoundwa kushughulikia maombi hayo, waliobahatika ni watu 16.

Waziri Shamuhuna aliwatoa wasi wasi wananchi kuwa hakukuwa na upendeleo wa aina yoyote katika kuwapata wanafunzi hao na kila kitu kilifanywa kwa njia ya mtandao.

“Tumekataa suala la ujomba au ushangazi katika nafasi hizi, tumetumia mtandao kuwapata wanafunzi bora na hao ndio waliofaulu kutokana na masomo waliyoomba na sifa walizanazo,”alisema.

Alisema hivi sasa wanaendelea kuboresha masomo ya sekondari na hivi karibuni watakwenda Oman kuzungumzia suala hilo ili kupata wanafunzi wengi zaidi wenye sifa za kujiunga kupitia msaada wa Sultan Qaboos.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>