Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JWTZ Lavionya Vyombo vya Habari Vinavyopotosha kuhusu DRC.

$
0
0
Na Mwandishi wetu, DSM
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limevionya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vinavyopotosha ukweli kuhusu jukumu lililopewa na jamii ya kimataifa kusimamia amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa Jeshi, Meja Erick Komba aliwambia waandishi wa habari jana kwamba jukumu la kulinda amani DRC linapaswa kuungwa mkono na wote, vikiwemo vyombo vya habari.

Alivitaka vyombo vya habari kuweka uzalendo mbele badala ya kuandika taarifa za kupotosha ukweli.

Aidha alisema kwa kuzingatia kuwa kikosi cha Tanzania kiko chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya MONUSCO, inamanisha kuwa operesheni inayofanywa DRC ni ya Umoja wa Mataifa.

Alisema kamwe Tanzania haipigani na M-23 na haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo na ridhaa ya kikosi cha Ranzania kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu.

Aidha alisema Rwanda imesaidia kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha watu, vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>