Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

JK.Sio Kazi ya Serekali Kulipia Madeni ya Vyama vya Ushirika.

$
0
0
Na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete amesema siyo kazi ya serikali kuviokoa vyama vya ushirika kutoka kwenye madeni kwa sababu shughuli za ushirika ni za sekta binafsi na mali ya wanachama wenyewe.

Aidha, Rais Kikwete alisema ni jambo la kusikitisha kuwa makosa ya ushirika na wezi wa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika hatimaye yanabebeshwa vyama vya siasa.

Rais Kikwete aliwataka viongozi wa mikoa kuwasaidia wananchi ili kupata viongozi waadilifu na waaminifu na wala siyo wezi kama ilivyo sasa kwa vyama vingi vya ushirika.

Aliyasema hayo usiku wa kuamkia juzi, wakati alipopokea rpoti ya maendeleo ya mkoa wa Mwanza kwenye Ikulu ndogo mjini Mwanza kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.

Aliwaambia viongozi hao:“Tumewahi huko nyuma kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika. Nia ilikuwa kuvisaidia vyama hivyo na wanachama wake kujipanga upya na kupata uhalali wa kuweza kukopa fedha za kujiendesha shughuli zao. Lakini sasa, vyama hivyo, vimerudi kule kule kwenye madeni.”

Alitoa mfano wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani kama moja ya vyama vya ushirika ambavyo madeni yake yalilipwa na serikali lakini sasa kina deni kubwa zaidi kuliko hata lile lililolipwa.

“Wale watu wa Pwani walikwenda kukopa na benki moja ikakubali kuwapa fedha. Wameshindwa kulipa na ule ushirika nadhani utakufa. Njia bora kwa vyama vya namna hiyo ni kuviachia vife tu kwa sababu havina faida yoyote kwa mkulima.”

Aliongeza: “Vyama vya ushirika siyo mali ya serikali. Ni mali ya wanaushirika na hivyo ushirika ni sekta binafsi. Lakini hakuna shaka kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanatesa wananchi.

Wanakopa fedha kwenye mabenki lakini wanashindwa kuzirudisha fedha hizo na hilo linapotokea serikali inalaumiwa kwa hali hiyo.”

Alikuwa akitoa maelekezo yake baada ya kuambiwa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza cha Mkoa wa Mwanza kilikuwa kinakamilisha mpango wa kukopa kiasi cha shilingi bilioni saba kutoka Benki ya Raslimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununulia pamba.

Lakini aliwaambia viongozi hao: “Uamuzi wa kukopa ama kutokukopa ni wa kwenu. Nyanza ni mali yenu, wezi waliopata kukibebesha madeni chama hicho mliwachagua nyie wenyewe. Fedha ni zenu lakini hatimaye athari za makosa yenu yanaiathiri serikali na hata vyama vya siasa.”

“Kuna wakati viongozi wa Chama cha Nyanza walipata kuuza godown ya thamani ya shilingi milioni 600 kwa shilingi milioni 50 tu. Hawa ni wezi wa mchana wanaoiba kweupe. Wanaiba lakini wanataka serikali iwasaidie. kwa nini? Nadhani kazi yetu kama viongozi ni kuwasaidia wananchi kupata viongozi uadilifu na aminifu siyo wezi,” alisema na na kuongeza:

“Tatizo ni kwamba hata sisi viongozi tunakataa kuwashughulikia wezi kwa sababu hawa ni watu maarufu na wakati mwingine baadhi ya viongozi wanakula nao na jambo hilo limekuwa tatizo kubwa sana. Tunavifikisha vyama vya ushirika mahali ambako sina uhakika kama bado ni mali ya wakulima. Wakulima wanakutana na ushirika wakati wa kuchagua viongozi tu na baada ya hapo wakulima hawaonekani tena.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>