Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Benki ya Dunia YaazaKuusuka Mji wa Zanzibar.

$
0
0
Na Khamis Amani
BENKI ya Dunia (WB), inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa uboreshaji wa mji wa Zanzibar, ili uweze kuwa na haiba nzuri na kivutio kwa wakazi wa ndani na nje.

Mradi huo ujulikanao kwa 'Zanzibar Urbarn Services Project' (ZUSP) unatarajiwa kuanza muda mfupi baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, Abeid Juma Ali, aliyasema hayo ofisini kwake Malindi alipokua na kikao na waandishi wa habari.

Alisema mradi huo utaleta mabadiliko makubwa ya haiba ya mji wa Zanzibar, ambao hivi sasa kuna kilio kikubwa cha serikali kutokana na hali yake isiyoridhisha.

Alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa mitaro ya maji machafu, michirizi, taka taka ambapo hivi sasa tayari wameshaanza kupokea vifaa mbali mbali kwa ajili ya usafi vikiwemo magari ya kusombea taka na vidampa vitakavyosaidia kurahisisha ufanyaji wa usafi.

Sambamba na huduma hiyo, mradi huo utahusisha ukarabati wa jengo la ofisi ya Baraza la Manispaa, ili liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Awali Mkurugenzi huyo alikanusha madai yaliyotolewa na wafanyabiashara wa soko la mboga mboga Mombasa, kuwa Baraza lilihusisha wanasiasa kwa ajili ya kuwaonea wafanyabiashara hao kwa kuwavunjia maeneo yao ya biashara.

Alisema kitendo cha uvunjaji wa maeneo hayo ni sahihi, kutokana na kwamba wafanyabiashara hao hawakupata ruhusa ya ujenzi kutoka Baraza ambalo ndilo lenye mamlaka ya kutoa ruhusa.

Alisema kibali walichopewa kimetoka kwa Mkuu wa soko ambaye kisheria hapaswi kutoa kibali, bali yeye alistahiki kumuarifu Mkurugenzi baadae Kamati ya Kazi, Ujenzi ya Baraza ambao wote hao walikuwa hawana taarifa.

Malalamiko ya wafanyabiashara hao waliyatoa katika kituo cha ZBC TV kwa madai wameonewa kwa kuvunjiwa maeneo yao na ilhali barua ya ombi la ujenzi waliliwasilisha kwa Mkuu wa soko hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>