Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Balozi Seif azindua chuo cha ushoni na ujasiri amali Kibweni

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha Ushoni cha wajasiri amali wa Kibweni kilichoanzishwa na Jumuiya ya Vijana wa Kibweni { Kibweni Yourth Organization  - KYO } katika Mtaa wa Kwa Botoro Kibweni Jimbo la Bububu.
 Balozi Seif akiangalia mmoja miongoni mwa wafanuzi wa chuo cha ushoni cha ujasiri amali kiliopo Kwa Botoro Kibweni mara baada ya kukizindua rasmi chuo hicho.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  akimkabidhi vyarahani Vitano Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Kibweni Kassim Ali ikiwa mchango wake kusaidia nguvu za nutendji Jumuiya hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi mzima wa Jumuiya Vijana ya Kibweni pamoja na wadau wao mara baada wa uzinduzi wa chuo cha Jumuiya hiyo cha Ushoni cha ujasiri amali kiliopo kwa Botoro Kibweni.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuanzisha Wizara inayosimamia  sekta  ya kazi  ni  kuhakikisha kwamba inapambana na tatizo  la ajira linaloonekana kuathiri nguvu kubwa ya Vijana hapa Nchini.
 
Kauli hiyo aliitoa wakati  akizindua rasmi  Chuo cha Ushoni cha ujasiri amali  kilichoanzishwa na  Jumuiya ya Vijana ya Kibweni { Kibweni Yourth Organization } kiliopo katika Mtaa wa Kwa Botoro Kibweni ndani ya Jimbo la Bububu.
 
Balozi Seif alisema hatua hiyo ya Serikali inakwenda samba mba na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 inayoelezea umuhimu wa kuundwa  kwa vikundi vya  ujasiri amali ambavyo hutoa fursa kubwa ya ajira miongoni mwa wananchi.
 
Alisema kazi za ujasiri amali zimekuwa zikisaidia kupunguza umaskini  na Serikali itajitahidi kuhakikisha inavijengea nguvu vikundi hivyo vya Jamii ili viweze kutekeleza majumu iliyojipangia.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jumuiya ya Vijana ya Kibweni kwa uamuzi wake wa kuanzisha Kikundi hicho ambacho ni mkombozi kwa wanajumuiya pamoja na vijana wa Jimbo hilo.

Hata hivyo Balozi Seif alihimiza viongozi na wana jumuiya hiyo kuwa wastahamilivu na kuvumiliana katika harakati zao za kila siku na hatua hiyo aliielezea kwamba itafanikiwa endapo utaratibu wa kufuata kanuni walizojiwekea utazingatiwa zaidi.
 
“ Nimefurahi kuona Vijana mmejikusanya kuanzisha mfumo wa ajira ambao Serikali kuu kadri ya hali itakavyoruhusu itazingatia na kutoa msaada unaostahiki ili kukiendeleza kikundi chenu “. Alisisitiza Balozi Seif.
 
Alihimiza mpango wa kuendelea kupanda miti ulionzishwa na vijana hao wa Kibweni ili kukabiliana na upungufu wa maji uliyoikumba nchi kutokana na tabia za baadhi ya watu kukata miti ovyo.
 
Katika kuunga mkono juhudi za Vijana hao wa Kibweni za kuanzisha Chuo cha Ushoni cha ujasiri amali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikabidhi Vyarahani vitano kama mchango wake wa kukipa nguvu Chuo hicho.
 
Balozi Seif pia aliahidi kuchangia Kompyuta moja na Mashine ya Kudarzi kwa chuo hicho hatua  ambayo imeungwa Mkono na Mwakilishi wa jimbo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu aliyetoa mchango wa Shilingi Milioni 2,000,000/- taslim wakati Mbunge wa Jimbo hilo Masoud Sururu ambae ndie mlezi wa Jumuiya hiyo akaahidi kuchangia Vyarahani Vitano, Pasi na Vifaa vidogo vidogo.
 
Akisoma  Risala ya wanajumiya hiyo ya Vijana wa Kibweni  mmoja wa mwanachama wa Jumuiya hiyo Farida Juma Haji alisema Vijana wa Kibweni wameamua kuanzisha  jumuiya hiyo wakitambua kwamba Serikali Kuu haina fursa ya kutoa ajira kwa watu wote.
 
Alisema elimu ya ujasiri amali ambayo ni muhimu kwa taifa lolote Duniani ndio itakayowapa nafasi pekee ya kukabiliana na tatizo hilo la ajira na upande mwengine jumuiya imelenga kwenda sambamba na mpango wa Taifa wa kupunguza Umaskini Zanzibar { Mkuza }.
 
Mapema akikikagua chuo hicho cha Ushoni cha ujasiri amali cha  Kibweni Mwalimu  wa chuo hicho Bibi Subira Haji Yahya alimueleza Balozi Seif kwamba lengo la kuanzishwa kwa chuo ni kuwajengea mazingira ya ajira vijana wa Shehia hiyo.
 
Bibi Subira alieleza kwamba mfumo huo wa mafunzo mbali ya kutengeneza kazi za ajira lakini pia utasaidia kupunguza wimbi la vitendo viovu wanavyojihusisha zaidi vijana ndani ya mitaa na kuleta kero na fadhaa kwa jamii.
 
Chuo cha ushoni cha ujasiri amali cha Kwa Botoro kilichoanzishwa na jumuiya ya Vijana wa Kibweni { Kibweni Yourth Organization – KYO } kimeanzishwa karibu miezi Tisa iliyopita kikiwa na wanafunzi 16 wa rika mbali mbali.
 
Wanafunzi wa chuo hicho hupata fursa ya kujifunza ushoni wa nguo tofauti wakianzi na zile za watoto wadogo kwa hatua ya ukataji na kufuatia ushoni utakaoambatana na kupatiwa vyeti wakati wanalizapo muda wao wa mafunzo.
 
Uongozi wa chuo hicho pia umeweka utaratibu wa kuwarahisishia wanafunzi wake muda wa mafunzo kulingana na harakati zao za maisha za kila siku ambapo pia hupata wasaa wa kujifunza lugha ya Kiingereza pamoja na upandaji miti katika maeneo ya vianzio vya maji vya Mwanyanya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>