Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kongamano la Kumbukumbu ya Miaka Miwili ya Kuzama kwa Mv Spice Zanzibar.

$
0
0

Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee akifungua Kongamano la Kumbukumbu ya miaka miwili ya kuzama kwa meli ya Mv Spice na mwaka mmpja wa kuzama kwa Mv Skaget Zanzibar, Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar.

Baadhi ya Waathirika wa ajali ya kuzama kwa meli ya mv spice wakiwa katika kongamano hilo wakifuatilia mada zilizowakilishwa na watowa mada kuhusiana na majanga ya maafa Zanzibar.

Waandishi wa  habari wakimsikiliza Wairi wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf akifungua Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar. katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi wa Maafa Zanzibar Ali Juma kazungumzia Taasisi yake ya Maafa jinsi ya kupambana na matatizo yanatokea katika maeneo ya Zanzibar jinsi walivyopambana na Maafa ya kuzama kwa meli za Mv Spice na Mv Skaget
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Abdi Omar, akitowa mada yake kuhusiana na udhibiti wa Vyombo vya Baharini na ukaguzi unavyofanyika kwa vyombo hivyo na kuelezea mapendekezo yaliotolewa na Tume ya Uchunguzi wa Kuzama kwa Meli za Mv Spice na Mv Skaget,
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Bahari Zanzibar Abdi Omar akiwasilisha mada yake kuhusiana na mambo ya Mamlaka hiyo inayokuchukwa kwa kupasisha Vyombo vya Bahari na ukaguzi wake na kuthibiti upakiaji wa abiria katika boti na vyombo vingine vya usafiri wa baharini.
Mwandishi wa habari mwandamizi Rashid Omar akiuliza swali kuhusiana na jitihada za kupambana na maafa Zanzibar na utaratibu wa kukabilianacna matatizo kama hayo indapo yatatokea.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar akichangia mada kuhusu ununuzi wa meli mpya inayotarajiwa kuwasili baada ya miaka miwili ijawi, kuwe na mponga wa meli hiyo kutumia kwa kusafirishia mahujaji Zanzibar, kuna baadhi ya Wananchi wanahitaji huduma hiyo ya kutumia meli kwenda hijja. 
Mwakilishi wa Kampuni ya Usafiri wa Bahari wa Kampuni ya Azam Marine Abdulrazak, akichangia mada katika Kongamano hilo kuhusiana na udhibiti wa uingiaji wa Wananchi katika bandari ya abiria wa boti na jinsi ya kudhibiti uuzwaji wa tiketi kwa wananchi  na hujitokeza baadhi yao hutumia tiketi sio zenye jina la msafiri hali.


Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Fedha akifungua Kongamano la Kumbukumbu ya Ajali ya Mv Spice kutimia miaka miwili na Mwaka mmoja wa Mv Skaget.Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni Zanzibar, lililoandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar  WAHAMAZA.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>