Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Fuse ODG Afunika Onesho lake Dar.

$
0
0



                                      Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki
                                                        Mashabiki waliojitokeza wakishangilia
                                                                     Menina akifanya yake




MSANII wa muziki wa muziki wa kileo kutoka nchini Ghana Fuse ODG, Azonto amezikonga nyoyo za wapenzi wa burudani baada ya kuchanganya staili yake ya uchezaji Azonto pamoja na ile ya Kiduku ya hapa nchini.

Fuse ODG ambae anajulikana zaidi kama Azonto alipanda jukwanii majira ya saa tisa kasoro usiku baada ya wasanii wengine wengi kumaliza kutoa burudani.

Ilikuwa ni baada ya kupanda kwa kundi la Tip Top Connection huku likiongozwa na msanii Madee pamoja na msanii Chid Benz ambae aliimba nao kama msanii rafiki.

Baada ya kumalizika kwa shoo hiyo kwa wasanii hao wa hapa nyumbani ndipo alipopanda msanii Azonto ambae alisikika akihamaisha kwa kutajan maneno ya kiswahili kama vile, Nawapenda, Mambo vip na piga kelele.

Msanii huyo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwaweka karibu zaidi wapenzi wake wa burudani hasa pale alipowapandisha jukwaani vijana wawili kucheza nao Azonto na Kiduku.

Alianza kwa kuwachezesha Azonto na kisha muda huo huo aliwabadilishia muziki na kucheza nao kiduku huku mwenyewe akiahidi kuiendeleza zaidi staili hiyo.

Akizungumza baada ya onesho hilo alisema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo wasanii na watu wa Dar es salaam walivyompokea na kuahidi kuwa ataiendeleza staili ya kiduku nakuitangaza zaidi.

"Mimi kwanza niliwahi kuja Tanzania na kufikia kule Arusha kwa mapumziko na kwa sasa nimekuja kwa kazi na nipo tayari kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kwani mwisho wa siku sisi ni waafrika ambao tunatakiwa kusaidiana na kuendelezana" alisema Azonto.

Wasanii kama vile Madee, Tunda Man, Water Chilambo, Menina Atik, kundi la Navy Kenzo, B Heats, Mabeste, Eskide, Mapacha na wengineo wengi pia walitoa burudani safi siku hiyo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>