Na Khamis Mohammed, Beijing
KUWEPO kwa vyombo huru vya habari na vyenye kuzingatia maslahi ya umma, kumetajwa kusaidia kuinua maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliopo hivi sasa nchini China ..
Profesa, alisema, pamoja na wajibu wa vyombo vya habari katika kuburudisha, kuelimisha, kukosoa au kutetea, lakini pia vina wajibu wa kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kutokana na nafasi iliyonayo kwa taifa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.
Alisema, programu za aina mbali mbali za kuelimisha jamii ya Wachina na dunia kwa ujumla zimekuwa zikitayarishwa kupitia telesheni ya taifa ya CCTV , hali ambayo imeweza kufikia wananchi wengi hata wale walioko vijijini.
“China ina magazeti 1943 ambapo magazeti 816 ni ya kila siku, ni fursa kubwa kwa wananchi katika kupata habari”, alisema Profesa Yan.
Aidha, alisema, mbali na wingi wa magazeti, China ina idadi kubwa ya vituo vya televisheni vipatavyo 360 vikiwa na chaneli zaidi ya 2000 ambazo huangaliwa na watu zaidi ya milioni 900.
Akuzungumzia rushwa kwa vyombo vya habari, Profesa Yan, alisema, China imekuwa ikipambana na aina zote za rushwa na kwamba serikali ipo makini mno katika vita hivyo.
“Wapo watu wameshahukumiwa mpaka adhabu ya kifo kwa kujishughulisha na rushwa na wengine kutumikia viungo vya muda mrefu, hii yote ni kuonesha jinsi serikali inavyokerwa na rushwa”, alisema.
Aidha, alisema, vyombo vya habari vimekuwa vikifichua aina ya vitendo vya rushwa na kuitaja kashfa ya maziwa yaliokuwa na sumu mwaka 2008, kwamba ilifichuliwa na vyombo vya habari.