MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Abdulhakim Haji Hafidhi, akifunguwa mkutano na Wadau wa Mfuko wa ZSSF kuimarisha na wadao hao kujuwa wajibu wa kulipa Mafao ya Wafanyakazi wao katika Mfuko huo, mkutano huo umewashirikisha Wadau kutoka Taasisisi za Serekali na za Binafsi Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar
Mwanasheria wa ZSSF akitowa mada kuhusu michango kwa Wafanyakazi kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Jamii Zanzibar, kwa Taasisi mbalimbali, Zanzibar kuwachangia Wafanyakazi wake katika mfuko huo, kwa ajili ya Mafao yao wakati wa kustaafu kazi.
Afisa Uhusiano wa ZSSF, akitowa elemu ya Uendeshaji na ukusanyaji wa Mafao ya Wafanyakazi kwa ajili ya kujiwekea akida ya Uzeeni ili kuja kuwasaidia, mkutano huo umezishirikisha Taasisi mbalimbali za Serekali na Binafsi kuwahamasisha kuchangia katika mfuko huo kwa Wafanyakazi wake.
Wadau wa Mfuko wa ZSSF wakifuatilia mada zinazowakilishwa katika mkutano huo kuwahamasisha Wadau kuchangia katika mfukon huo ili kuweza kuwawekea hakiba ya Uzeeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Jamii Zanzibar, Abdulhakim Haji Hafidhi, akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa ZSSF baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.