Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Chuo cha Diplomasia Chapongezwa kwa Kupeleka Taaluma Zanzibar.

$
0
0
Na Othman Ame, OMPR
UONGOZI wa Chuo cha Diplomasia cha Jijini Dar es salaam umepongezwa kwa hatua zake ulizoanza kuzichukuza katika harakati za kusaidia taaluma ya masuala ya Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alitoa pongezi hizo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar alipozunguma na Uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Mkuu wa chuo hicho Balozi Dk. Mohammed Maundi uliofika Zanzibar kwa hatua za awali za namna ya kuanza mpango huo.

Balozi Seif ambae aliwahi kutoa ombi hilo wakati akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya Tano ya chuo cha Utawala wa umma Machi 30 mwaka huu huko Tunguu, alisema taaluma hiyo inaweza kusaidia wanafunzi hao wanapoamua kuendelea na mafunzo yao katika ngazi za Kimataifa.

Alifahamisha kwamba dunia hivi sasa ina mfumo wa mazingira ya kutegemeana hivyo ni vyema kwa watumishi wa umma pamoja na wanajamii kuanza utaratibu wa kujipatia taaluma inayofanana na mazingira hayo ya Ushirikiano wa Kimataifa.

“ Nimefurahi na kushukuru kuona kwamba lile wazo langu nililolitoa kwenye mahafali ya chuo cha utawala wa Umma Zanzibar mapema mwaka huu limeanza kutoa matumaini mazuri ambayo kwa kweli yananipa moyo mkubwa “, alifahamisha Balozi Seif.

Balozi Seif alieleza kuwa taaluma hiyo ikienea zaidi miongoni mwa jamii italenga kukomaza mfumo wa uhusiano wa Kidiplomasia hapa nchini.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Dk. Mohammed Maundi, alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi wa chuo hicho unajiandaa kuleta wataalamu Zanzibar ili kuangalia na kuona hatua za pamoja za kuchukuliwa katika muelekeo wa pamoja na chuo cha Utumishi wa Umma wa kuanzisha mitaala ya mafunzo ya diplomasia.

Balozi Maundi alisema ipo haja ya kubadilishana mihula ya wanafunzi kati ya vyuo hivyo ili kuongeza ushirikiano kati ya wanataaluma wa Chuo cha Diplomasia Dar es salaam na wale waChuo cha Utawala wa Umma hapa Zanzibar.

“ Tunaweza kuanzisha mafunzo ya pamoja miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vyote viwili. Hii itasaidia pande zote husika kwa vile uwezo wa walimu wetu unaweza kutumiwa na pande zote mbili “, alifafanua Balozi Maundi.

Alisema chuo cha Diplomasia hivi sasa kiko katika mchakato wa kuanzisha kiwango cha Digirii ya kwanza kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi wanaoomba kujiunga na chuo hicho ambao wengi wao wanatokea Zanzibar.

Mkuu huyo wa Chuo cha Diplomasia anayehusika zaidi na fani ya usuluhishi katika migogoro ya rasilmali asilia, alimshukuru Balozi Seif kwa wazo lake lenye mustakabali wa kuwajengea uwezo zaidi wa kitaaluma wanafunzi wa Zanzibar.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>