Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa Ardhi Makazi Maji na Nishati Ramadhani abdalla Shaabani amesema Jumla ya hati 344 zimetolewa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba ambapo hati 35 kwa ajili kilimo na 309 kwa ajili ya makazi.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la wa kilishi wakati alipo kuwa akisoma kitabu chake cha bajeti ya Wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013-2014 mwaka ujao
Amsema ametoa hati hizo kwa kuwapa fursa wananchi kuwapatia makazi na kuimarisho kilimo ikiwa ni sehemu ya uendelezaji maisha ya mwanadamu akiwa hai.
Amesema muendelezo wa utoaji wa hati hizo pia ulifuatana na zoezi la kubadilisha hati za zamani na kuwapatia wananchi hati mpya za kisasa na kupokea hati za zamani 105 na kubadilishwa kwa kuwapa wahusika hati mpya .
Aidha waziri huyo akielezea malengo yao kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa za wizara na kusimamia utekelezaji wakazi za wizara kwa ufuatiliaji na kutathimini miradi kumi ya maendeleo ambayo ni pamoja na ,usambazaji wa maji na usafi wa mawzingira .
Nyengine kuimarisha mradi wa mindo mbinu ya maji mkoa mjinimagharibi na kuijengea uwezo mamlaka kifedha ,na uhuwishaji na upanuzi shghuli za maji mijini na vijijini .
Pia kusambaza umeme vijijini,uimarishaji wa miundo mbinu ya umeme unguja na pemba ,ufungaji wa mita elfu 20 za tukuza, utekelezaji sera ya nishati ,utafiti nishati mbadala, usimamizi endelevu wa aridhi na mazingira.
Vilevile kukuza kuimarisha uhusiano baina ya Wizara tatu za SMT na washirika wa Maendeleo na kuratibu matayarisho ya sera ya mipango miji na kukamilisha mapitio ya sera ya ardhi na sera mbali mbali za wizara.